Aslay: Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu

Interest

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2015
Posts
3,434
Reaction score
7,072


Mwanamuziki Aslay Isihaka kutoka katika kundi la Yamoto Band amefunguka na kuweka wazi kuwa anasumbuliwa sana na watoto wa kike ndiyo maana ameamua kuweka mahusiano yake wazi, Aslay alifunguka hayo alipokuwa akichat Live katika kipengele cha Kikaangoni Livekupitia ukurasa wa facebook wa EATV.

Aslay alisema kuwa moja ya sababu iliyomfanya kumuweka wazi mpenzi wake huyo ni kutaka kutoa ujumbe kwa wale ambao wanamsumbua kuwa waache kufanya hivyo kwani tayari ana mtu ambae yeye anampenda.

"Nimeamua kuweka mahusiano yangu ya mapenzi wazi sababu nasumbuliwa sana, nahisi kufanya hivyo wataelewa na kuacha, yaani kama nimewapunguzia speed ya usumbufu"

Mbali na hilo Aslay aliweza kuzungumzia juu ya elimu yake na kusema hakuacha shule kwa sababu ya muziki ila ataendelea na shule pale alipoishia, ilaa anaamini atafanya hivyo siku za usoni.

MAHUSIANO YAKE NA WEMA
Tetesi zilizopo mtaani ni kwamba Aslay Isihaka alikuwa akifukuziwa na Wema Sepetu kimapenzi na watu wengi walipouliza swali walitaka kufahamu ukweli juu ya suala hilo na ndipo hapo Aslay alipofunguka na kuweka wazi juu ya suala hilo na kusema kuwa hakuna ukweli wowote na wimbo wa Nitakupwelepweta hajaimbiwa Wema Sepetu.

"Watu wanakuwa wanaongea mambo mengi juu ya maisha yangu hususani katika mahusiano na kusambaza taarifa zisizo na ukweli, mfano watu wanasema natoka kimapenzi na Wema huo siyo ukweli kabisaa bali Wema ni kama dada yangu, ila kutokana na mambo haya ndipo niliamua kuweka mahusiano yangu wazi ili kila mtu ajue kuwa nipo kwenye mahusiano na mtu fulani na waache kusambaza taarifa zisizo na ukweli."

Kwa kifupi hizo taarifa wanazosema mashabiki hazina ukweli wowote,kwa sasa nimemtangaza mpenzi wangu na ndiye niko nae, sitaki usumbufu tena kwa sasa.

Chanzo: EATV
 

Attachments

  • WEEEE.jpg
    27.9 KB · Views: 2,193
Baadhi ya mademu wa bongo movie akili zao zipo makalioni,hivi inamake sense kweli Naima wa clement kuwa na uhusiano na Aslay? Wema si anamzaa kabisa Aslay? Naima kwenye video ya mbagala 2009 alivyo limama halafu muangalie Aslay wa 2010 nakusemea kwa mama!! Mademu wa Bongo ukiwa na kaumaaruku kunuka utawakimbia ebu mcheck mtu kamkumbatia kaka akahojiwa na Clouds hivi sasa anawalamba tu maselebriti tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…