Aslay: Ukijua unachofanya raha sana...

Aslay: Ukijua unachofanya raha sana...

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
Aslay-tete.jpg

Nimeshindwa kujizuia nimeona nitie neno kidogo kuhusu huyu dogo baada ya kusikiliza mapini yake non-stop.

Kwanza kabisa hakuna kitu kizuri kama kufanya kitu unachokipenda na uwe unakijua, huyu dogo anajua ndio maana hatumii nguvu nyingi kuwashawishi watu waukubali muziki wake, hahitaji kutengeneza 'kiki' ili watu wasikilize muziki wake, hahitaji kuomba interview XXL ili azindue wimbo wake, media tour sioni kama huwa anafanya kabla hajaachia wimbo, yeye kazi yake ni moja tu kuweka wimbo u-tube na kwenye instagram then raia wanaufatilia, hahitaji kufanya video ya mamilioni yeye anajiamini na tuvideo twake twa laki 5 na ndo tunampatia views zaidi ya milioni.

This is the next BIG THING kwenye bongofleva!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Enok na beka wanaweza pia

Yule mwimba bes arud kuimba kwaya

mchana toch ,usiku magogo tufanyaje?
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Unaota.

Diamond anakwambia alitoa 'Kesho' akiwa amelenga soko na ni kati ya ngoma ambazo hazipendi kwa kua haipo katika mahadhi yake.

Unamsifia Aslay jamaa ambaye najua kua ataanza kwa sauti ya chini huku biti ikiwa na vyombo vichache na vitachanganya kidogo kidogo huko mbele, cheki Muhudumu, cheki Angekuona, cheki Rudi, Cheki Tete, cheki Likizo, cheki Baby, cheki Koko, cheki Danga, cheki Danga remix zote muundo ni ule ule.

Asipobadilika anapotea, tangu nijue muziki sijawahi sikia msanii anatoa ngoma mfululizo zaidi ya nne kwa mara moja yeye katoa zaidi ya 14.
 
Mi nadhani katoa nyimbo nyingi mfululizo ili awe nazo za kutosha kupigia show, itafika wakati atatulia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana nyimbo nzuri, ila angekuwa akitoa anaiacha nyimbo inafika kwenye peak yake ikianza kushuka ndio atoe nyingine. .

Namtabiria makubwa, ana mashabiki pia. . Hasipojua kuwatumia na kuwa na njaa ya kufika mbali, atabaki hivyo hivyo tunaburudika na ngoma zake afu chali
 
Mi nadhani katoa nyimbo nyingi mfululizo ili awe nazo za kutosha kupigia show, itafika wakati atatulia

Sent using Jamii Forums mobile app
Aslay ana nyimbo nyingi hata kabla ya hizi, kabla ya Ya Moto Band yeye alishakua ana airtime kwenye radio kupitia hizo nyimbo.

Sababu yako siyo ya ukweli.
 
Namkubali sana ila anahitaji ushauri wakufanya mziki wa kibiashara zaidi umlipe. Business skills zinahitajika kwenye gemu, akifyatua tu kama tofali bila kuangalia faida ila kupendwa itakula kwake. Anahitaji mwongozo atoke hapo alipo, sijui level ya shule yake ila kipaji anacho.
 
Unaota.

Diamond anakwambia alitoa 'Kesho' akiwa amelenga soko na ni kati ya ngoma ambazo hazipendi kwa kua haipo katika mahadhi yake.

Unamsifia Aslay jamaa ambaye najua kua ataanza kwa sauti ya chini huku biti ikiwa na vyombo vichache na vitachanganya kidogo kidogo huko mbele, cheki Muhudumu, cheki Angekuona, cheki Rudi, Cheki Tete, cheki Likizo, cheki Baby, cheki Koko, cheki Danga, cheki Danga remix zote muundo ni ule ule.

Asipobadilika anapotea, tangu nijue muziki sijawahi sikia msanii anatoa ngoma mfululizo zaidi ya nne kwa mara moja yeye katoa zaidi ya 14.
Ni hivi ndugu yangu, hawa vijana unajua walikuw bend , ila kwasasa ni kama bend imeyumba kidogo kwahiyo wameambiwa kila mwenye uwezo atoke kivyake, means watoe nyimbo zao na show itakuwa kila mtu kivyake, sasa aslay asipotoa nyimbo nyingi show atapiga vipi? mana hana single za kutosha kufanya show, ofcoz lazma atoe nyimbo nyingi asipotoe nyimbo huko kwenye show ataimba nini? au ulitaka akiitwa kwenye show akaimbe nyimbo za bend?
 
Ukiangalia show ya komaa concert Beka alitumia muda mwingi kuimba nyimbo za wasanii wengine, hayo ndo madhara ya kutokuwa na nyimbo nyingi. Mwenzake Aslay ni bandika bandua

Wacha waseme - Aslay & Abamto
Mugogo - Aslay
Kasema mama - Aslay
Nakusemea - Aslay
Utachezaje - Aslay
Maneno - Aslay & Ali Nipishe
Bado mdogo - Aslay & Lina
Niwe nawe - Aslay
Wananitesa - Aslay
Siwezi - Aslay
Kengele - Aslay
Kikombe cha babu - Aslay
Umbea - Aslay

Hazitoshi kufanya show hizi? Hapo sijaweka za mwaka huu mwanzoni.
 
Back
Top Bottom