favouredman
Member
- Nov 15, 2024
- 21
- 38
Umeanguka Babeli.
Umeanguka binti sayuni. Ulitarajiwa kuwa furaha kwa wengi lakini harufu ya kidonda chako imeongezeka. Uchungu wako umezidi, ghadhabu na ukali wa upole wako vinatisha.
Nzi wengi wamekuandama kidonda chako, na hakika hakitapona. Uliingia kwa huruma na kiu yako imezidi huruma ile. Mikono yako imejaa damu. Harufu ya maovu yako haivumiliki tena.
Vilio, huzuni, uchungu na hasira vimesikiwa malangoni kwako. Ulionekana kuwa na haki na sasa haki haipatikani kwako. Utaanguka binti sayuni. Mlango ule ule ulioingilia ndio utakaotokea. Kama Alivyoanguka Babeli mkuu ndivyo utakavyoanguka ee binti sayuni.
'Mungu pamoja nasi' ataketi. Naam ataketi maana hofu imeonekana kwake, hofu ya haki na amani yatawala kwake. Kiti chake hakitaondolewa. Jifunze kwake eeh Binti sayuni ili usitiriwe maovu yako kabla ya kuezuliwa kwako.
Asomaye na Afahamu.