Asante sana kwa maelezo mazuri na yenye upendo ndani yake. Umeni-boost confidence yangu zaidi. Kabisaa, huwa pia sipendi mbwembwe nyingi zisizo na sababu. Ngoja leo nijaze hiyo ya ajira portal kwanza niwasililizie. Maana iko nafasi moja but I feel confident to try it.2. Kuhusu kwingine ambako unatakiwa uandae CV inayojitegemea bila ya kujaza taarifa zako kwenye mfumo, uwe na amani sana. Ma Hr, huwa wanatudanganya kupita maelezo, kwa kutuambia mbwe mbwe nyingi kuhusu uandishi wa Cv, mpaka inafika hatua watu wanakuwa na wasiwasi juu ya namna ipi ni sahihi kuandika Cv.
Ukweli ni kwamba andaa Cv yako kwa standard inayoeleweka na isiyochanganya, punguza manjonjo na urembo, kikubwa kinachoangaliwa sio namna ulivyoiremba au kupanga, suala ni, “Je unavyo wanavyovitaka?”
Kama unavyo vinavyohitajika, viweke vionekane kwa urahisi, kisha jiandae kuvitetea kupitia kuandika na kuongea.
Afrika mkuu Ina mambo yake ya kipekee😀. Asante sana kaka, nafanyia kazi haraka!.1. Ajira portal maelezo unayoweka kutokana na sehemu unazotakiwa kujaza ndiyo yanatengeneza CV automatically. Hivyo huna haja ya kuumiza kichwa kuhusu utaandika nini au kwa mpangilio gani kwenye Cv.
Nimeshangaa madogo walioomba ajira TRA, walitakiwa kujaza taarifa za kina kisha wakatakiwa tena kupandisha na CV inyojitegemea, kitu ambacho ni kufanya kazi moja mara mbili, na sio kweli watakaozipitia watapitia zote mbili.
NB: Nikakumbuka hii ni Afrika, tunafanya mambo yetu kinamna yetu.