Assumption: Mahojiano ya wakili na Mkuu wa wiliya ya Ubungo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Cross Examination Day;

Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ijuze mahakama kiwango chako cha elimu.

Mkuu wa Wilaya:
Shahada

Wakili:
Ieleze mahakama majukumu yako kwa kifupi

Mkuu wa Wilaya:
Mwakilishi wa Mhe. Rais Wilaya ya Ubungo na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya

Wakili:
Je! Unawafahamu madada 36 walioko hapa mahakamani

Mkuu wa Wilaya:
Siwafahamu

Wakili:
Ilikuwaje ukaamuru Polisi wawakamate na kuwashikilia mahabusu?

Mkuu wa Wilaya:
Ni 'madada Poa'

Wakili:
Mhe. Mkuu wa Wilaya ieleze mahakama unamaanisha nini unaposema hawa ni 'Madada Poa?'

Mkuu wa Wilaya:
'Madada Poa' ni wanawake wanaojishughulisha na biashara haramu ya kuuza miili yao.

Wakili:
Je! Ulijuaje madada hawa wanafanya hiyo biashara uliyoisema?

Mkuu wa Wilaya:
Niliwakuta wamesimama usiku Sinza

Wakili:
Je! Ulipowakuta walikuuzia wewe miili yao

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Unaweza ukataja majina ya wateja (wanaume) waliokuwa wananunua miili ya hawa madada?

Mkuu wa Wilaya:
Sikuwaona.

Wakili:
Unafahamu maana ya biashara

Mkuu wa Wilaya:
Biashara ni shughuli ya kuuza na kununua bidhaa au huduma

Wakili:
Je! kusimama Sinza usiku ni kufanya biashara

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Kusimama Sinza usiku ni kosa la Jinai?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Je! Unafahamu kuwaita madada hawa jina ulilowaita na kuwaweka kwenye Vyombo vya Habari ni kuwadhalilisha na kutweza utu wao mbele ya waume zao, familia zao na umma kwa ujumla (Defamation)?

Mkuu wa Wilaya:
Ndio

Wakili:
Je! Unafahamu kuwakamata watu na kuwashikilia rumande Polisi kwa muda wa ziadi ya siku tano pasipo kuwapeleka mahakamani ni kinyume cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Sura 20?

Mkuu wa Wilaya:
Najua

Wakili:
Kwa hiyo umefanya makusudi kuvunja Sheria za nchi?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana. Nilikuwa nasafisha Wilaya yangu ya Ubungo

Wakili:
Je! Unamaanisha hawa madada ni takataka?

Mkuu wa Wilaya:
Hapana

Wakili:
Mhe. Hakimu sina maswali zaidi
 
Aisee! Mbona unamsanua tena huyu mshenzi apate abc za maswali ya cross-examination? Mwache apuyange mwenyewe mjinga huyu!
 
Licha ya kwamba mkuu wa Wilaya kajichangaya takribani kwa kila swali aliloulizwa mahakama haitomfanya chochote. Sio mda hii kesi itageuka kiini macho.
 
Back
Top Bottom