balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,771
- 14,294
Nimeamini neno kwaheri ni gumu sana,ni gumu kupitiliza pale unapolazimika kulitumia baada ya Kufika tamati ya jambo,kitu au mtu uliyempenda.Maisha ya mwanadamu yana milima na mabonde ,mengi huvukwa,watu wakapanda mlima huu na kushuka mlima ule,kuna milima mingine ni mgumu sana na mwanadamu hushindwa kuivuka hivyo kuamua hatima ya jambo lao flani hata kama bado wakilihitaji.Hatima ya jambo ni kama muda,waswahili Wana wahenga wao na wahenga walishasema wakati ni ukuta,kama wakati ni ukuta,nani huweza kupiga mgumi ukuta?Hapa namkumbuka Zinedine Yazidu Zidane,nguli huyu wa soka,katika mechi Moja ya mwisho kabisa ya Kombe la Dunia pale Ujerumani 2006, alikasirishwa na mtoto mtukutu wa pale Torino,Marco Materazzi,Zizzou akamtandika bonge la kichwa na mwamuzi akamlima Zizzou kadi nyekundu huo ukawa mwisho wa Kombe la Dunia kwa Zidane na Ufaransa ikalikosa kombe.Ubabe huu wa Zidane haukufua dafu mbele ya wakati pale ilipombidi Zizzou kutundika daruga,akahitimisha muda wake kama msakata kabumbu.Ndugu yetu Yona Phares Maro( RIP),hakupata ujasiri wa kusema kwaheri akaendelea na maisha mengine ,alichomudu ni kujikamua uhai kwa kuona amesalitiwa.Ronaldino Gaucho ulituburudisha wengi na sasa umeamua kutuaga,hatutakuona tena ukizungusha gozi la ng'ombe uwanjani ingawa unaweza kudumu Katika Dunia ya soka kama mwalimu au wakala lakini hii haitarudisha enzi zako Dimbani.Kibaya zaidi kwetu na kwako pia ,bado hajapatikana kama wewe,mtu aweza sema Neymar jr lakini huyu mtu ana uzuri wake lakini hakufikii Gaucho,ulikuwa sukari,asali na hata grisi kwenye vyuma.Hakika ulitutendea haki mtu wewe.Kumtazama Gaucho,ilikuwa sawa na Kumtazama Beyonce ,Jlo au Elizabeth Michael akiwa mtupu kitandani huku mkuyenge ukiwa unadai haki yake.Hapohapo unalazimika kusema kwaheri ingawa nilikupenda sana,siwezi kupambana na ukuta.Unaishia kusema tu,mimi nyumba ya udongo,sihimili vishindo.ASTA LA VISTA.