Asthma ya ngozi

ram

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Posts
9,326
Reaction score
8,505
Kwenu madaktari wa JF, nina swali eti kuna Asthma ya ngozi?

Mtoto wangu anatatizo la kutoka rashes/vipele mwilini na vikimtoka vinamuwasha sana, nilimpeleka hospital tofauti tofauti akawa anaandikiwa dawa za kupaka lakini baadaye daktari mmoja akaniambia mtoto ana tatizo la ngozi so mpeleke kwa specialist wa ngozi, nikampeleka kwa specialist wa ngozi, ajabu, baada ya kumuangalia tu akasema mtoto ana asthma ya ngozi, nilishangaa kweli, akamuandikia mafuta fulani hivi ya kupaka ambayo yanatengenezwa hospital ya KCMC tu. ALiendelea vzr lkn kwa bahati mbaya sijawahi kubahatika kumuona tena huyo specialist, na yale mafuta yalishaisha, nilienda kwenye ile hospitali nikaomba nipewe tena yale mafuta kwa bahati mbaya sana wakasema yameisha.

Naombeni msaada wenu kama kuna dawa mbadala,manake kwa sasa vipele vikitoka nampaka diplosalic oitment ambayo pia inamsaidia kwa sehemu lakini pia naona kama atakuwa ni mtu wa kupaka hiyo dawa tu maisha yake yote, kwani hapaki mafuta mengine yoyote, siku moja moja tunampaka Vaseline Blue Seal ile isiyo na harufu

Nawasilisha
 
Asthma ya ngozi ni allergy au tunaita atopic dermatitis, ugonjwa huu unarithiwa kama asthma. Na family yenye asthma mara nyingi inakuwa na ugonjwa huu pia. Mtu mwenye asthma ya ngozi mara nyingi anakuwa allergic to animal protein zote. Hivyo basi dawa zote utakazo tumia zitakuwa za kutuliza tu kikubwa ni kuepukana na vyakula vinavyomsababishia kuwasha. Hii tulishadiscuss sana humu jf, natumia cm kuandika hapa vidole plz ni pm namba yako nikucall
 
Ahsante sana Barca, nitakupa namba yangu soon, tanks sana na MUngu akubariki
 

aisee nami kijana wangu ana hilo tatizo kama utanisaidia itakuwa poa sana
 
nina jirani yangu pia ana mtoto ana hilo tatizo na walimwambia ana athma ya ngozi,hebu wekeni hapa jamani tuwaelekeze na wengine!!!!
 
na mimi niku PM namba yangu unitumie hela?
 
Mimi nina athima ya ngozi nimegundulika mwaka jana baada ya kuwa navimba sana mwili na kuwashwa ila kwa sasa sina shida sana nilienda kumuona DR aga khan now sina shida kabisa

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
kwa watoto wadogo kuna uwezekano wakapona baada ya muda fulani...around 2 or 3 mpaka 5 years hivi.
kama una mtoto anayesumbuliwa na huu ugonjwa mara nyingi ngozi yake huwa kavu na yenye itching. Hakuna dawa ya tatizo hili ambayo itaponya moja kwa moja na mara moja. Lakini unaweza kumsaidia mtoto kuwa katika hali ya kawaida kwa kuifanya ngozi yake iwe oily muda mwingi, na utafanya hivi kwa namna hii.
changanya maji ya kumuogeshea mtoto na Virgin Olive Oil, siyo ujaze sana bt weka kiasi, pia waweza tumia mafuta ya Ubuyu na pure Sunflower Oil.
mafuta ya kumpaka pia ni ya kuchagua as Vaseline will not do good to her/him.
I will come up na maelezo zaidi ya mafuta na namna ya kumtunza kuanzia mavazi nk, ngoja niatend meeting moja kwanza.
 
Reactions: ram
Ahsante mpendwa, nakusubiri

 
ESZCEMA ni ugonjwa wa kawaida sana kwa watoto wa dogo haswa katika mwaka wao wa kwanza wa kukua..nadhani huyo daktari alikupa corticosteroid ointment.There are 4 groups of corticosteroids which kategorize how strong the medication.
I-is the weakest group
IV-is the strongest
Jambo la muhimu ni kutibu inavyotakiwa kwa wiki moja coz hutakiwi utumie dawa hizi haswa kwa watoto kwa zaidi ya wiki inaweza kusababisha ngozi iwe fragile na kumbuka mtoto bado anakuwa kwahio ngozi yake haijawa completely developed.
USHAURI:
Lazima kuna factors zinazosababisha huo upele jaribu kuepuka na jaribu kuchunguza:
1.fulia sabuni ambayo haina harufu
2.usitumie vipodozi vyovyote vyenye harufu kwa mtoto(powder,sabuni ya kuogea)
3.tumia nguo za cotton only
4.Mpake HYDROCORTISON KWENYE UPELE(sio umshindilie,important to have a thin layer),kisha unampaka na vaseline isiyo na harufu baada ya kumpaka hio HYDROCORTISON OINTMENT
Hio hydrocortison ni Group I(the weakest) nashauri ujaribi hio kwanza!
 
Ahsante mpendwa, nakusubiri

Hello ram, nimerudi upya!tatizo la mwanao waweza ukapunguza makali yake kwa kufanya hivi.
1.Tumia sabuni muafaka kwa ngozi yake
2.Tumia mafuta muafaka
3. Mvalishe nguo zinazoruhusu hali yake!
Tuananze kimoja kimoja!
Soap;
Tumia sabuni ambazo ni for sensitive skin,
For this purpose I will recommend utumie Dove extra Sensitive au Dove Cream Oil (supreme).
Pia waweza tumia aina nyingine yaitwa Simple Cream Bath au Simple Soap! (Sabuni zote hizi waweza zipata kwenye Super Market kubwa kubwa hapa DSM.
2. Oil/Mafuta
Wakati wa kumuogesha changanya maji ya kuogea na Virgin Olive Oil. Fanya circulation ya Olive Oil na Mafuta ya Ubuyu au Pure Sunflower oil.
Usimpake mafuta kama Vaseline as itasababisha ukavu wa ngozi and Hence mtoto kuwashwa. Hakikisha unapompaka hiyo Olive Oil au mafuta ya Ubuyu ngozi ya mtoto iko wet (ina maji after kumuogesha)
3.Nguo
Usimvalishe mtoto glittering cloth, make sure nguo zote anazovaa sio nguo zenye kuwaka in terms of colour. Ukiwa unapata nguo ambazo ni 100% cotton ni nzuri zaidi.
Nafikir ram na wadau walioni-pm nimewajibu.
If condition is severe u can apply hydrocortisone ointment 1% just for short time,then condition iki-improve acha kutumia and do kama nilivoelekeza hapo juu!
Mwisho naamini atakayefuata nilivoelekeza ataona matokeo mazuri kwenye ngozi ya mtoto!
 
Last edited by a moderator:
Kamanda Moshi ahsante sana kwa ushauri wako, nitafanya kama ulivyonishauri mpendwa, naamin tatizo la mwanangu litakwenda kupungua kama sio kwisha kabisa. Nawashukuru hata wadau wengi mlionishauri juu ya tatizo la mwanangu, Mungu awabariki sana.
 
Last edited by a moderator:

Pole sana. Sijui mwanao ana umri gani. Natumaini wadau wengine watakusaidia kwa ushauri.

Niliishi na huo ugonjwa tangia nikiwa na umri wa miaka miwili hadi nilipofikisha umri wa miaka ishirini. Tulitembea almost Tanzania nzima kutafuta dawa. Tulipita kwa wanganga wa hospitali na waganga wa miti shamba. Na mtu wa kwanza kugundua nina asthma ya ngozi ni mganga wa mitishamba alikuwa anaishi shinyanga mbali mno na mjini, akanipa dawa nikatumia, nikapumzika kuumwa kama miaka miwili. Baadae ugonjwa ukarudi tena, yule mganga akawa hajulikani alipo.
Mwisho tulikwenda kumuona Professor Masawe Hapo muhimbili(sijui kama bado yupo),baada ya kufanya utafiti wake alituambia hakuna dawa isipokuwa ugonjwa utapungua kadri ninavyoongeka umri na utatokomea kabisa nikifikisha umri wa miaka 20. Isipokuwa aliniambia nisile samaki, nitumie sabuni ambazo hazina kemikali za kukarabati ngozi yani sabuni za kawaida zisizo za urembo, pia mafuta nitumie pure petroleum jelly,na kweli ugonjwa ulipungua mno kiasi kwamba nilikuwa sihisi kitu.

KCMC nilikwendaga nikalazwa, nikawa natibiwa na dokta mmoja toka Ujerumani alinipa dawa ambazo pia ziliniponyesha kwa miaka miwili na hizo dawa alikuwa nazo yeye tu Tanzania nzima, hata baadae ugonjwa ulivyorudi nilienda KCMC kumuulizia yule dokta nikaambiwa amerudi kwao na zile dawa ni za kwake alikuja kuzifanyia research.
Sikupenda yale majibu kwa sababu niligundua wazungu wanakuja kufanya majaribio kwenye miili yetu sisi watanzania, ningetambua hili mapema ningegoma kutumia dawa zake.

Angalizo
Usichanganye madawa ya hospitali na ya mitishamba, nilikiona cha moto, yalinilaza kitandani ndugu wamezunguka kitanda changu hawajui cha kufanya, ilikuwa nikivuta hewa kifua chote utadhani kimewekwa mikuki ndani kinachoma ajabu, ilibidi niwe napumua taratibu mno ili maumivu yasiwe makali.
 

Hongera kwa kupona. Mie inaibuka ukubwani sasa sijui ndio ntapona nikiwa 80 mwe. Ntafuata ushauri though!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…