Astrazeneca yaondoa chanjo yao ya Covid-19 (Astrazeneca Covid-19 Vaccine) kwenye Soko la Dunia

Chanjo mbaya ila ARVs ndio sahihi? Chanjo ya manjano na homa ya ini ni halali? Ila ya Covid pekee ndio makosa?

Kwa akili hizi no wonder CCM inatawala
Hakuna aliyepinga chanjo, suala lilikuwa kwamba hizo chanjo zilikuwa za haraka sana kuanza kutumika kwa binadamu ndani ya muda mfupi na bila kuwa na majaribio ya muda mrefu na kujiridhisha usalama wake kwa watumiaji. Kuna kesi nyingi za kuomba fidia kutokana na madhara yaliyosababishwa na chanjo za COVID hasa kwa nchi za Ulaya.

Hizo ARVs na chanjo nyingine na zenyewe zilichukua kipindi kifupi kutengenezwa kama hizo za COVID?
 
Muda mrefu miaka au miwezi mingapi?
Sijawahi kuwaona wenye akili waliopinga chanjo yoyote.
Wabongo tukikosa hoja tunakimbilia kwenye kuwa na akili au kutokuwa na akili. Kila mtu ana akili na ana matumizi tofauti ya akili zake.
Hoja ya msingi ni kwamba pamoja na sayansi na teknolojia chanjo za COVID ziliharakishwa na baadhi ya vitu vilikuwa hyped.
Ndo maana baadhi ya nchi kama UK waliona ni upuuzi kuendelea kufungia watu na kulazimisha watu kuchanja wakatoa masharti yote ya COVID na maisha yakaendelea kama kawaida.
 
Magufuli aliikataa hiyo chanjo leo hii astra zeneca anakiri kuwa chanjo hiyo ina side effects hatari zinazohatarisha uhai wa mtu kaamua kuiondoa ili alinde credibility ya kampuni anahofia kukosa uaminifu.
Nitajie chanjo au dawa yoyote duniani ambayo haina side effects? Hata JPM alikua anatumia pacemaker ambayo side effects ndio kama hizo unapigwa shoti ya umeme!! Mbona hakuacha kutumia?

Hata ARVs za ukimwi zina side effects kwanini JPM hakuzikataa? Ile mionzi ya MRI scan au ya radiotherapy mbona zinaside effects kubwa ila hazipigwi marufuku Tanzania?

Ni ujinga kupinga chanjo ya Covid alafu unatumia chanjo za saratani ya titi na Hepatitis B
 
Hizo ARVs na chanjo nyingine na zenyewe zilichukua kipindi kifupi kutengenezwa kama hizo za COVID?
NDIO, chanjo ya ebola ilichukua miezi michache tu ikaanza kutumika mbona hamuipingi?
Kuna kesi nyingi za kuomba fidia kutokana na madhara yaliyosababishwa na chanjo za COVID hasa kwa nchi za Ulaya
Exactly kama ambavyo kuna madai ya fidia kwa chanjo za homa ya ini, ARVs na madawa mengi tu tena yaliyofanyiwa tafiti kwa miaka mingi.
Hoja ya msingi ni kwamba pamoja na sayansi na teknolojia chanjo za COVID ziliharakishwa na baadhi ya vitu vilikuwa hyped
Sasa watu walikua wanakufa ulitaka wafanyeje? Tokea chanjo imeletwa kelele za Covid ziliisha mpaka leo kwahiyo ilikua success. Sasa mnaacha kufocus kwenye success rate ya kuokoa vifo mko busy na side effects!! Kwamba ni kheri mtu afe kuliko apewe chanjo apate side effect minor?
suala lilikuwa kwamba hizo chanjo zilikuwa za haraka sana kuanza kutumika kwa binadamu ndani ya muda mfupi na bila kuwa na majaribio ya muda mrefu na kujiridhisha usalama wake kwa watumiaji.
Okay so mbadala ni nini? Wangeachwa watu wafe mpaka waishe? Wewe kama ungepewa kazi ya ushauri ungeshauri nini kipindi kile?
 
Kwa afrika kulikuwa hakuna ulazima wa kukurupukia chanjo kwa sababu mazingira ya Ulaya na Afrika ni tofauti wala hata hayakaribiani.
Kuhusu vifo kwa upande wa afrika nahisi vilikuwa exaggerated baada ya kuripotiwa vifo vingi nchi za Ulaya. Kwa hiyo point kwamba watu wangeachwa wafe haina mashiko yoyote kwa sababu afrika COVID haikuwa tishio kwa maisha ya watu kama maralia, ajali za barabarani na magonjwa mengine.
 
Mkuu zitto junior watu walikataa chanjo za covid 19 sababu ya kufupishwa muda wa mchakato wa kuipitisha chanjo kama inafaa na haina madhara.
Nimesoma alichoandika huyo jamaa... Sijaelewa anachotaka kujustify kuhusiana na kuondolewa kwa chanjo hizi SOKONI.....
 
COVID-19 - USA weapon of Mass destruction of human kind. Magufuri alikuwa hili watu wakamudhihaki sana, leo wazungu wanapita mule mule. Hizi sindano zimeua watu wengi sana duniani. Wengine wamekuwa vilema wa kudumu. Harafu mijamaa imetengeneza billions of dollars kutokana na ujinga wa binadamu.


View: https://youtu.be/D1t4KYNjHPY?si=Y3yH8AuguqFwvBRBCOVID-19 USA biotech military cartel


View: https://youtu.be/morj-3rdWwM?si=X_KTSiEt7Ej09wfz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…