Wengi humfahamu Marijani Rajabu kama mtunzi na muimbaji, lakini alikuwa pia mpiga gitaa mahiri, kama anavyoonekana katika video hii wakati yuko katika kundi lililokuwa na staili wakiiita 'Mahepe Ngoma ya Wajanja'. Hii ni clip fupi kati ya nyingi zitakazoonekana katika kipindi cha TV kitakachoanza kuwa hewani karibuni ili kuhifadhi historia ya sanaa zetu Tanzania.(JOHN KITIME)
Leo nimeshinda kutwa nikisikiliza nyimbo zake hasa @pendo si la kulazimishana@.Nimewawekea wanangu nikawauliza kuhusu mtiririko wa kisa chenyewe na wote walimkubali.
Hakuimba nyimba ya kipuuzi,zote ni za kuelimisha tangu akiwa trippers.
Mungu Amsamehe makosa yake na amuweke peponi,Aamin.