Senior Bachelor,
ingawa ujumbe wako umeuelekeza kwa Ndetichia, nina uhakika ulikuwa ukilenga kunijibu mimi.
Nashukuru kwa maelezo yako..ni kweli nimetumia tafsiri hiyo makusudi.
Ila nina swali dogo tu: Je, ni wakati gani unaofaa/usiofaa kufanya direct-translation? maneno mengine unaweza usijue kwamba yana hidden truth kama hilo nililotumia hapo juu, "Turn back the hands of time". Kwangu ni neno very straight na ndo maana nikadhani linafaa kutafsiriwa directly as opposed to 'a chip off the old block'.
**Inje lya kurun..nimeielewa pia kwani ni lugha yangu!lol
Ndugu Mentor,
Nashukuru kwa kuni"tonya" kuwa nilimjibu Ndetichia wakati nilidahmiria wewe! Naye pia namuomba radhi kama nitakuwa nimemkwaza.
Tafsiri sisisi unaweza kuifanya pale ambapo italeta maana inayoeleweka. Kwa mfano nikisema "Mentor went to school"-hapo ni kuwa "Mentor alienda shule". Hakuna lugha ya picha hapo. Ni lugha ya moja kwamoja. Huwezi kuifanya kwa lugha ya picha (figurative language). Mfano nahau, methali, misemo, n.k.
Hebu fikiri nikienda mahali nikamwambia mtu "natamani kurudisha nyuma mikono ya wakati". Kama huyo mtu haujui huo wimbo wenye maneno hayo, au hajawahi kuusikia huo msemo wa kiingereza hawezi kukuelewa. Kwanza, wakati (time) hauna "hands". yenye "hands" ni saa (clock). Na hands of a clock tunaiita "mishale" ya saa na wala sio "mikono" ya saa. Kwa hiyo "hands of time" inaonesha wazi kuwa ni nahau. Sasa ndugu Mentor nahau za lugha 2 tofauti haziwezi kufanana sawasawa kama hivyo (labda mara chache sana). Yaani zifanane hadi mpangilio wa maneno! La hasha. Heri hata ungesema "kugeuza/kurusidha nyuma mishale ya saa". Kidogo ingevumilika japo sio sana.
Kwa hiyo: Tafsiri sisisi haifai kwa nahau hata kidogo. Achilia mbali kutoka lugha moja kwenda lugha nyingine. Hata kwa lugha hiyohiyo tu kama nilivyosema huwezi kupata maana kwa kutumia maana za neno moja mojaa. Ukienda katika kamusi ukatafuta maana ya kila neno katika nahau hiyo halafu ukayaunganisha utaishia na maana ya ajabu (absurdity).
Mfano mdogo: Fikiria mgeni anayejifunza kiswahili akutane na sentensi zifuatazo zikiwa zimetumiwa kisanii (lugha ya picha) halafu atake kujua maana yazo kwa kwenda kwenye kamusi na kutafuta maana ya maneno yake halafu akaunganisha. Lol! ataishia na vitu vya ajabu sana.
1) Kumwaga unga
2) Kwenda mwezini
3) Kuvunja ungo
4) Kujikaza kisabuni
5) Kula kobisi (naamini sasa ni nahau rasmi)
6) Kuachwa solemba (naamini pia ni nahau sasa)
7) kujivua gamba (nayo pia ni nahau mpya
Tafakari.