Atafutwe Kocha mbunifu zaidi Taifa Stars

Daniel Mwinula

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2012
Posts
302
Reaction score
328
Ni jambo la kheri na la kutia moyo kuona nchi zetu za Afrika Mashariki zimechaguliwa ku-host mashindano ya AFCON. Hapo tunatakiwa kujiandaa kwa vitu vikubwa viwili, VIWANJA BORA na TIMU BORA….!!!

Binafsi ningetamani sana atafutwe kocha MAPEMA mwenye uwezo wa kubadilisha kabisa mpira wetu tuliouzoea, na kujenga timu bora itakayoweza kuleta changamoto CHANYA katika mashindano hayo…!!!

Naamini kocha mgeni mwenye kariba ya kocha Nabi (kwa mfano), anaweza kusaidia kujenga timu vizuri sana endapo atafanikiwa kukaa na timu kuanzia mapema. Nimesema Nabi kwa sababu ni ukweli usiopingika kwamba Nabi alijitahidi kuleta changamoto fulani TOFAUTI na tulivyokuwa tumezoea.

Au combination ya mgeni na mzawa kama Mgunda, binafsi naamini kwa muda uliobaki wanaweza wakatengeneza timu INAYOELEWEKA, huku tukiamini kwamba wachezaji waliopo kwa sasa UMRI UNAELEKEA KUWATUPA MKONO….!!!

Wapewe kazi ya kufanya scouting ya kutosha kutafuta vipaji vipya na kupika timu mpya nzuri kwa muda wa miaka mi3 iliyobaki INATOSHA KABISA….!!

Yangu ni hayo tu….!!!
 
Shida ya mpira wa Tanzania sio makocha shida ni wachezaji, tuna rundo la wachezaji ambao hawana misingi mizuri ya mpira tangu mwanzoni, ndio maana hata hatuna wachezaji wazuri walio tokea kwenye ligi yetu wakaenda kufanya vizuri wanako enda, hata akiletwa Pep wa Manchester city bado atashindwa kwa wachezaji tulio nao
 
Aisee mkisha kula viporo kwa shemeji na kukaa kwenye sofa huku umenyoosha miguu na kunyamba mnataftaga visa visivyo na kichwa wala miguu

Kocha huyuhuyu ameikuta team inapumulia mtungi ICU akafumua akawatoa kina Tshabalal,Kapombe vilevile akaleta madogo damu inachemka wamekiwasha pamoja na ubovu wa timu wamefuzu Afcon wako mbioni kufuzu CHAN bado tu unaropoka ushubwada shenzi kabisa
 
Dah! Jamaa yangu kenge umetumia maneno makali sana.
 
Nafikiri Kenya na Uganda baada ya kujua wataandaa afcon wameshaanza kuandaa mikakati ikiwemo kutengeneza timu itakayoshiriki hii michuano, sisi so ajabu tukawa tunawekeza kwa kina Msuva na Kibu Dennis
 
Uwe na shukrani. Uliona mechi ya kifuzu dhidi ya Algeria. Mwalimu alitumia ufundi wa Hali ya juu kushinda ile mechi.
 
Hilo wa sio shida ya mpira wa tanzania

Shida ya mpira wa tanzania ni
.
WACHEZAJI KUTOJITAMBUA

wapo wapo tu ilimradi siku ziende, akinunua harrier na akijenga nyumba ya vyumba vinne anaona tayari amemaliza

Kwa kifupi hawana njaa ya mafanikio makubwa wameridhika na kuchezea simba na yanga.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hivi kunakuaga na ratiba kweli, ambayo wakati mechi za vilabu zinasimama labda kwa wiki moja au zaidi, hatakama hakuna mechi ya taifa angalau kocha kuita wachezaji wake wa kitaifa na kufaya mazoezi nae , kubadilishana mawazo angalau kwa siku 2 au 3?
Maana naona kocha wa taifa anaenda kuteua wale wanaofanyishwa mazoezi na makocha wa vilabu vyao.kuwaita hadi itokee mechi ya kitaifa tu.
 
Daaah mwanang endelea kuandika, yaani ulikuw unataka kusema nini hapa😅😅, endelea....nakusikikiza kwa makini😅😅
 
Uwe na shukrani. Uliona mechi ya kifuzu dhidi ya Algeria. Mwalimu alitumia ufundi wa Hali ya juu kushinda ile mechi.
Kabisa mzee, kwanza aliwaambia algeria kuwa mnajua mimi ni ndugu yenu? Wakajibu ndiooo, basi msiniharibie kibarua changu
 
Timu apewe Gamond wa Yanga![emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…