Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,336
- 4,731
James Msengi Mkazi wa Tabora anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 40 amenusurika kifo baada ya kujaribu kujiua kwa kujikata na kisu shingoni akiwa kwenye kituo cha Mabasi cha Msamvu mkoani Morogoro.
Majeruhi huyo ambaye amesema alikuwa anasafairi kutoka Dar es salaam kuelekea kwao Tabora lakini alipofika katika kituo hicho cha mabasi aliamua kujikata kwa makusudi shingoni kwa lengo la kujiua kutokana na ugumu wa maisha ambao ulisababishwa na kukosa ajira.
Katibu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Scholastika Ndunga amethibitisha kumpokea Majeruhi akiwa katika hali mbaya na kutokwa na damu nyingi shingoni ambaye alianza kupatiwa matibabu na sasa anaendelea vizuri.
Shuhuda wa tukio hilo Mzee Ibrahim Omary ambaye Majeruhi alitumia kisu chake cha kuuzia miwa kujikata koromeo amesema kuwa Mtu huyo alifika katika eneo analofanyia biashara na kutaka auziwe muwa ambao haujamenywa lakini walishangaa baada ya kupewa kisu akaanza kujichinja.