Atakaenisaidia hili nitampa Tsh Milioni moja taslimu

Status
Not open for further replies.
Maelezo yako yanavuta matapeli wazidi kukuibia kwa sababu kichwani kwako umeamini kulogwa. Umesema nyie ni maskini, sasa hao watu wawaonee wivu gani kwa raha gani miliyonayo hapa duniani. Ninakuomba ueleze kinagaubaga unaumwa kitu gani, yaani aidha kichwa hakiponi, tumbo au kiungo gani hasa na maumivu yakoje. Mimi sio mwumini wa dini ya USHIRIKINA, bali yako mambo mengine ni ya kimila tu. Nitakupa mfano mmoja. Dada mmoja alizaliwa katika familia maskini lakini Mungu akamjalia kupata elimu na bahati nzuri enzi za Mwalimu elimu ilikuwa bure mpaka upeo wa akili yako, hivyo yeye alipata elimu ya chuo kikuu. Alianza kazikama Mwalimu na na muda mfupi baadaye akajenga nyumba yake ya kisasa ya kuishi kijijini kwa wazazi wake, akajaliwa kupata mtoto wake wa kwanza lakini yule mtoto alimtesa sana mama yake kwa kuugua kila wakati. Yule dada alizunguka mahospitali mengi pasipo mafanikio na vipimo vyote havikuonyesha maradhi yanayomsibu mtoto. Mwisho aliamua kwenda kwenye tiba mbadala (kienyeji) na bahati nzuri alikutana na mtu sio tapeli na wala hakumpa dawa yoyote bali alimwambia kuwa huko kwenu kuna mtu japo wewe humfahamu alifariki wakati wewe hujazaliwa, alikuwa anaugua ukoma, huyo mtu analalamika kuwa wewe ni kizazi chake umefanikiwa katika maisha na umejenga nyumba nzuri, hivyo na yeye anaomba ukamjengee nyumba. Yule binti alifunga safari hadi kwa wazazi wake na kuliulizia hili, aliambiwa ni kweli kuna mjomba wake huyo dada, yaani kaka wa mama yake alikufa zamani kwa ugonjwa wa ukoma na wakampeleka kwenye kaburi lake. Alichofanya ni kununua cement na kuajiri mafundi wakajengea kaburi la huyo Mjomba na kufanya sala kwa imani ya dini yake. Basi kuanzia siku hiyo tatizo lake lilikoma na mtoto hakuugua tena.
 
Soma biblia kuhusu mold kwenye,Leviticus 13:47-59 NIV, g'day.
 
Pole. Leo naenda kwenye maombi mahali fulani. Nitumie jina lako kwenye pm ili niende nalo pale. Mungu wetu ni mwema naamini utakuwa mzima tena. Na hiyo hela yako utamtolea Mungu sadaka ya shukrani.

Mimi jina langu ni CCM usinisahau kwenye maombi, nina pepo la wizi na ufisadi.
 


Ni sawa huo ni mtazamo na maono yako jinsi unavyolitazama na kuliangazia suala hili ila kwa uzoefu wangu wa miaka zaidi ya 19 juu ya hili tatizo nimejifunza mengi sana sana tu. Pia suala la ulozi halijitanabaishi sababu ya mali hapana ni hofu yao tu wandugu hawa juu ya harakati za familia yetu kwani mtaa mzima hali zetu kiuchumi sio za kuridhisha sana ila kwetu tunajituma sana kufanya kazi na kutumia fursa za mtaa vizuri.baaasi!!

Ila nisingependa kuzungumza mengi bali nieleze tu ninavyoumwa na kuusikia mwili kwanza kichwa kinauma sana hadi nafikia hatua ya kutokuwa naconcertrates kwa makini, tumbo linauma as if kuna kitu kinatembea ndani, mwili .unachemka joto sana, kifua kinabana, mwili unanyong'onyea, mikosi ya ajabu ajabu n.k
 

Nipe namba ya simu au email yako tuwasiliane.Yaliyokupata yanafanana na yaliyonipata,nimeteseka miaka 6 lkn kwa kudra za mwenyezi Mungu akanifungulia,nikikumbuka machozi yananitoka!
 

wewe upo wapi then dont believe about witch doctor
 
Nipe namba ya simu au email yako tuwasiliane.Yaliyokupata yanafanana na yaliyonipata,nimeteseka miaka 6 lkn kwa kudra za mwenyezi Mungu akanifungulia,nikikumbuka machozi yananitoka!

Pole sana ndugu!! Unajua wanasema "kisichokuua kinakufanya unakua imara zaidi" mshukuru mungu kwa kukuepushia kikombe hicho mapema!

Bila shaka natuma mawasiliano yangu kwako sasa.
 
Unapata haja kubwa Kama mbuzi mkuu? Na inatoka kwa shida?wakati mwingine mpaka unapata hemorrhoids na kusababisha damu kuvuja sehemu ya haja kubwa! I have been through hell mkuu, Tumbo linaunguruma? Ni kwasabab mold wame host ur digestive track and kills all good bacteria! Mwili unakosa virutubisho! Bila kuua mold kwa antifungal therapy na kutumia probiotic mfumo wa uyayushaji chakula hautafanya kazi Abadan, inaonyesha familia yenu yote mmekuwa kuwa exposed na mold pengine mnatofautiana symptoms ila wote wagonjwa.
 

Binafsi nafarijika ninaposoma chambuzi zako makini, murua na za kisomi zaidi kaka!! Hatuwezi jua yaweza kuwa mold kweli!! Kuna haja ya kutazama na hii mold!!
 
Dawa ndogo ama mkoa naomba milioni yangu
 
Dawa ndogo ama mkoa naomba milioni yangu

Inauma sana unajua ndugu, mtu unapokuwa serious halafu mtu anakuja anakejeli!!

Ila binadamu hatuwezi kuwa sawa, nakushukuru pia wewe nae kwa hilo.
 
Poleni sana, nafikiri kwa kuanzia Pima, white blood cell count, cortisol level, tostestorone level na anemia inawezekana familia yenu Ina carry gene Kama Mimi, you're all sensitive to mold bila kutibiwa itakuwa ngumu kufanya maendeleo bila afya hakuna maendeleo mkuu hata Kama labda uwezo wa kupata matibabu nje ya nchi ni mgumu, jaribu kuongea na daktari atayekuwa tayari kujaribu ushauri wangu na atakuwa ana wa monitor mtakavyokuwa mnaendelea, ila lazima mhame kwanza mnapoishi.
 
Folk pamoja na maombi, na dawa za mzizimkavu kwanini usifuate ushauri wa sokwe kupeleka sample US? Amekuambia atakuunganisha na Dr. kuhusu kutuma sample inawezekana ukifuata utaratibu.

Huyo shetani au devil au mchawi, hutumia vitu vilivyoumbwa kukuroga; sasa huenda katumia hao fungus kukuletea yote hayo na Mungu hutumia watu kuleta neema, yaweza kuwa mchngaji au madaktari wa US.
Check na sokwe, amelikomalia hili kwakuwa anakuonea huruma kwani alikuwa kama wewe ndio maana anakuelewa kuliko sisi wemgine.
 
Last edited by a moderator:
Bora kaunga unisaidie, this guy and his family are sick and I do believe, they're all suffering from mold, it takes years for mold to breakdown your body to that extent, unahisi vitu vinakutembea hiyo ni muscle spasm inayosababishwa na hizo toxins mwilini, Mimi nilipata severe hair loss nakuonea huruma sana.
 

Vyema kwa vyema kaunga. umejenga hoja thabiti hii, Nahisi kama kuna haja ya kuutizama ushauri wako kwa uzito unaostahili.pia sokwe ni mtu mzuri anaonekana.
 
Last edited by a moderator:

Tatizo lako ni ndg sana,inategemea uliombewa wapi na nani?sio kila mtu ana uwezo wa kuomba,wewe kama ni mkristo itumie damu ya Yesu itakuondolea yote hayo,nimeshuhudia watu walikuwa na matatizo makubwa kuliko yako sasa imebaki historia nitafute kwa 0762768053 (tuma text)nitakuelekeza utakapopata msaada bure wa maombi
 

Hiyo million moja nenda nayo kanisani ukatoe sadaka kwa mchungaji na matatizo yako ndiyo yatakuwa yamekwisha kuanzia siku hiyo. Matatizo katika uimwengu wa roho hayatafutiwi solutions "mechanically" kama unavyojaribu kutaka kufanya wewe hapa. Give it a trial and you will tell me!
 


Rudi kanisani uombewe maombi ya mnyololo au maombi ya waombaji ambao wanafunga kwa ajili yako. nina amini ya kuwa utapona kwani wenye matatizo kama yako sasa wamepona na wanayashuhudia matendo makubwa ya Mungu Baba.Kama upo dar njoo Ubungo Kibangu muone Mchungaji Ananja nina hakika Mungu atakuponya kupitia Mtumishi wake hyo.
 
Nina uwezo wa kumsaidia mtu huyu wagonjwa wa aina hii wanaongezeka sana.tatizo alilonalo ni moja kati ya magonjwa ya akili.na wengi wenu humu jammii forum mnayo so kwa msaada ni pm niwapatieni utabibu.shukran na karibuni.
 
Mkuu umenifikirisha sana hapa,hayo niliyo bold nahisi hunipata mara kwa mara,niambie sasa hao mold mazingira yao ni yepi? One border of my house used to be a clean stream ,now all the garbages in liquid form passes near my crib, do not let me explain the smell!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…