Atakaye shinda kalenga ana haki ya kuingia bunge maalum la katiba ..?

Atakaye shinda kalenga ana haki ya kuingia bunge maalum la katiba ..?

Maganga Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2009
Posts
2,089
Reaction score
829
Wadau kwa yeyote mwenye ufahamu anaweza kusaidia hili ni wazi kampeni za uchaguzi mdogo zimeanza huko kalenga na tamati yake 15.3.2014 ambapo 16.03.2014 utafanyika uchaguzi wenyewe ..

sasa swali langu ni je mbunge atakaye chaguliwa atakuwa na haki kisheria kuhudhuria bunge la katiba..?

kama ndio ataapishwa na nani..?

na kama jibu ni HAPANA si itakuwa ni kuwanyima haki wana kalenga uwakilishi..kwenye hili BM ..?
 
Kuwepo kwa Bunge la Katiba hakumaanishi kufa kwa Bunge la Jamhuri.
Hivyo ni wazi kuwa ataapishwa ktk kikao cha Bunge la Jamhuri.
 
Kama ikishinda ccm ataingia hili bunge la katiba na atalipwa posho zoote kuanzia siku wenzake walipo anza kuzilamba kwani huko ni posho tu zinaangaliwa.
Akiwa ni wa chama chochote cha upinzani, zengwe atakalo wekewa hata pale mlangoni hafiki. Mpaka Bunge lirudi mwakani kwenye bajeti. Mark ma word labda asiwepo Lukuvi
 
Kwa kuwa ni bunge la katiba ataapishwa na M/kiti wa hilo bunge kama mjumbe wa bunge la katiba kisha tena baadaye ataapishwa na Spika mara tu bunge la JMT litakaporejea kama mbunge wa JMT anayeiwakilisha Kalenga!
 
Back
Top Bottom