Atakayeiongoza CHADEMA 2025-2030 atapitia misukosuko mingi sana ya visasi vya kisiasa katika kuimarisha na kudhibiti chama

Atakayeiongoza CHADEMA 2025-2030 atapitia misukosuko mingi sana ya visasi vya kisiasa katika kuimarisha na kudhibiti chama

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Na hii ni pamoja na hujuma za makusudi kutoka kwa wanachama, wapambe na viongozi wa mgombea wa kambi pinzani watakaokuwemo uongozini.

Infact, bila umakini kwenye hili, chadema will be no more in Tanzanian political scene.

Watatumia kila aina ya mbinu kukwamisha malengo na mipango mahususi ya chama ili kumpaint kiongozi atakaechaguliwa kana kwamba kashindwa uongozi.

Kutakua na kufukuzana chamani kusiko koma, lakini pia wanachadema wengi kujiengua na kujiunga na vyama vingine vya siasa kwa visingizio na sababu mbalimbali, na hili litakua ni jambo la kawaida sana kwa uongozi wa chadema unaokuja.

Uongozi ujao,
ni uongozi ambao hautakua na amani kabisa, na hali hiyo inaweza kua hivyo katika kipindi chote cha miaka mitano au vinginevyo. Lengo ni kuhakikisha anaeshika uongozi wakati huu hapati utulivu, fursa wala nafasi ya kufanya kazi na mambo ya maana ndani ya chama kwa kipindi chote atakachokua uongozini, ili hatimae aje awajibishwe kwenye uchaguzi wa Taifa unaokuja. Kazi kubwa itakua ni kuonyana na kufukuzana tu chamani.

Hata hivyo,
uropokaji unaweza kuongezeka zaidi ndani ya chadema na kutuhumiana mambo ya uongo vikaimarika sana ndani ya chama, huku collective responsibilities kulingana vikao vya kikatiba vikaonekana ni kama ushirikina tu.

Hali hii ya minyukano na visasi vya kisiasa, ubabe, malumbano, uhasama, kutuhumiana na kurushiana vijembe vya nguoni vya kisiasa baina ya wanao tafuta uongozi hususan wa kitaifa, isipotulizwa na kudhibitiwa kisiasa inaweza kuleta athari kubwa kwa chadema, na pengine athari zikawa mbaya zaidi ya zile ziliyowahi kuvikumba vyama vya NCCR Mageuzi ya hayati Lyatonga Mrema na James Mbatia, lakini pia zile zilizokikumba chama cha wananchi CUF.

Kwa kifupi,
hapatakua na utulivu wa kiuongozi Chadema baada ya uchaguzi wa Jan.21.1.2025.

Na kwenye uchaguzi mkuu wa Oct 2025, hali inaweza kua mbaya zaidi ndani ya chadema kuliko wakati mwingine wowote, na hili nitalifafanua kisayansi na kitaalamu zaidi, wakati muafaka 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Na bado lazima uandike sana propaganda mwezi huu dhidi ya Chadema.

Waambie tu CCM watulie msiempenda ndo huyo anakuja.
kwahiyo umeandika nini sasa gentleman 🤣

umekunywa chai au bado?
nenda kanywe chai kwanza plz 🤣
 
Una maana ccm itawafinyia figusu hadi waombe poo?
 
Una maana ccm itawafinyia figusu hadi waombe poo?
soma vizur kwa utulivu bila mihemko gentleman,
itakusaidia sana kuongeza uelewa na ufahamu wako kuhusu mambo haya muhimu ya siasa hususan za ndani ya chadema 🐒
 
Back
Top Bottom