KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Wanachokifanya naona Kama mahubiri tu! Tushazoea ahadi zao kila siku ahadi ahadi ila hawana mstakabari wa ujibuji "KIVIPI?" Kila atakae mwaga ahadi ama sera zake ajibu atafanya hivyo kivipi? Atakayesema ataimarisha Uchumi ajibu kivipi ataimarisha uchumi wasituletee swaga!
Ifike hatua wanasiasa wawe ni watu wenye mipango iliyowazi ya kuitetea nchi.. njia zao ziwe wazi sio tu kunena jukwaani utaongeza mishahara lkn hujibu kivipi wakati huohuo unasema TRA utapunguza makusanyo ya Kodi!! Sasa hiyo hela ya kuwalipa watu utaipata wapi?
Tuwe serious hili si Jambo la chama fulani ni swala la nchi nzima bila kuangalia itikadi.. hata yule anaesema kutakuwa na ubwabwa huo ubwabwa inatakiwa ujibike kivipi? Nani atagharamia hizo gharama n.k
Ifike hatua tukue kifikra sio tu kubeba mabango ya vyama na kushabikia kisa umepewa ka elfu tano au tisheti ama kofia au chumvi!
Wananchi tukiwa serious viongozi watakuwa serious pia,maswala ya kwenda kuwachekea wakiwa jukwaani yaishe.. hizo ni ajira na wakiwa kwenye kampeni ni sawasawa na kusema wapo kwenye interview,hivyo si sehemu ya mtu kwenda kusema mambo yake bali atatumiaje vilivyopo nchini ili kufika malengo yetu na kivipi?
Hili swali kivipi lazima lijibike wawe wanataka au hawataki maana huwezi kuwa na swala then hujui utalitekeleza vipi..!
Kuwa hivyo ni sawa na kusema watu wanaenda kusikiliza kelele tu!
Baadae tunakuja kulaumiana tu tulimchagua fulani na hakufanya vitu!.. hakufanya kwasababu alikuwa hajui pia itavifanyaje hivyo vitu na hamkumuuliza ili mumpime,mkarubunika kwa vihadaa vya chumvi na kanga!
Tusipobadilika hakuna kitakachobadilika.. kwakuwa tunakubali watuhubirie yaleyale bila kuwa na KIVIPI? Tutapata yaleyale elimu duni,maji hola,umeme hola,Kodi lukuki,ajira hola,kilimo hola,ufugaji hola,viwanda hola kila kitu hola.