Anajihisi tu jamaa yako, mapenzi yanaweka kuwa very successful mwambie asiwaze mabaya tu awaze na mazuri kwamba atakuwa amemuoa mwanamke anaempenda kwa dhati, ila kama anaogopa kupandiwa kichwani na ameshaona dalili hizo, aonyeshe msimamo mapema kwa mwanamke wake asisubiri keshamdekeza wee ndio anaibuka na sheria zake
Inamkuta rafiki yangu...anashindwa kuchukua hatua
Msichana aliyempenda sana hapo awali na wakatengana kila mtu kuelekea njia yake toka mwaka 2008 anajisikia kumpenda sana na binti anaonesha nia ya kutaka kuwa nae kwa mara nyingine kuendeleza uhusiano.........
Anashindwa kuelewa, je akirudiana nae msichana atampenda na kuona kuwa yeye jamaa anampenda au atampanda kichwani kwa kuona hana pa kukurukukia pengine?
Nani amewahi kuona hali kama hii? Je huwa mahusiano ya pili thabiti zaidi au huzaa tatizo kama mmojawapo kumdharau mwingine? Mnasemaje katika hali kama hii?
Nawasilisha
Fanya umuoe. Kwenye ndoa ndio utapata majibu hayo hata hivyo kumbuka kuwa zimwi likujualo halikuli likakwisha. Kama bado anakukubali baada ya miaka hiyo ina maana kuwa bado anakupenda huyo lakini pia tizama kama hali yako kiuchumi imetengemaa kuliko mwanzo isije ikawa pia ni sababu. Peleka pendekezo la ndoa utizame mshindo wake
duh! title ya thread hii cjaielewa kabisa mkuu, hebu idadavue pls!