ATCL hawana ujuzi wa kuendesha biashara

IN SUMMARY

Katika mitandao ya kijamii ziliibu-ka hisia tofauti pengine hali hiyo ni kutokana na ATCL kutozindua safari zake kwenda Nairobi.Hata hivyo, mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi jana alisema shirika hilo linafanya biashara ya usafiri wa ndege hivyo si ajabu kuio-na popote. “Popote unapoona ndege yetu ina abiria au mizigo ujue tuna-fanya biashara,” alisema.

Dar es Salaam. Ndege aina ya Airbus A220-300 ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imekodiwa kupeleka watu Nairobi nchini Kenya kisha kuwarudisha na kuendelea na ratiba nyingine kama kawaida.

Juzi ndege hiyo yenye nakshi za rangi ya bluu na nyeupe, mchoro wa twiga kwa nyuma na maandishi yas-omekayo Air Tanzania The Wings of Kilimanjaro ilionekana katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta nchini Kenya.

Flight radar (programu ya kufua-tilia urukaji wa ndege) inaonyesha ndege hiyo iliruka katika Uwanja wa Jomo Kenyatta saa 12:00 jioni kabla ya kurudi nchini.Ukodishaji wa ndege kwa ajili ya kubeba watu au mizigo ni utara-tibu wa kawaida katika mashirika mbalimbali ulimwenguni na huin-giza fedha nyingi.

Katika mitandao ya kijamii ziliibu-ka hisia tofauti pengine hali hiyo ni kutokana na ATCL kutozindua safari zake kwenda Nairobi.Hata hivyo, mkurugenzi wa ATCL, Ladislaus Matindi jana alisema shirika hilo linafanya biashara ya usafiri wa ndege hivyo si ajabu kuio-na popote. “Popote unapoona ndege yetu ina abiria au mizigo ujue tuna-fanya biashara,” alisema.

Hata hivyo chanzo cha kuaminika kililieleza gazeti hili kuwa, ndege hiyo ilikodiwa na watu wa Airbus bila kubainisha kama ilichukuliwa kwa ajili ya maonyesho ya ndege (Airshow) jijini Nairobi au matumizi mengine.

Tanzania inamiliki Airbus A220-300 mbili na ni nchi ya kwanza barani Afrika kuwa na ndege hizo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni katika awamu hii tu watanzania kwa mamilioni wamepata maji safi na salama, habari kama hizi zipo nyingi na ndio maana 2020 hakuna mbunge wa upinzani atashinda

Umepata kibari cha kuanza kampeni za uchaguzi ujao ?
 
Kuna watu roho zinawauma wakiziona hizi ndege zinafanya vizuri, yaani wao leo wakisikia dreamliner imeanguka na kuua abiria wote inaonekana watafanya sherehe kubwa sana, upinzani wa aina hii upo Tanzania tu, mpinzani wa Nchi hii hana tofauti na gaidi
tatizo mnafanya mambo sirini, kama mnajua kuwa mnayoyafanya ni sahihi kwanini kuyafanya gizani? kama sio mange kufukua hili kaburi wala serikali isingekuja na huu utetezi wake
 
tatizo mnafanya mambo sirini, kama mnajua kuwa mnayoyafanya ni sahihi kwanini kuyafanya gizani? kama sio mange kufukua hili kaburi wala serikali isingekuja na huu utetezi wake
Hivi kumbe mpaka leo kuna watu mnamuamini huyo mwehu? Poleni.
 
Ni katika awamu hii tu watanzania kwa mamilioni wamepata maji safi na salama, habari kama hizi zipo nyingi na ndio maana 2020 hakuna mbunge wa upinzani atashinda

Hizo awamu nne zilizopita zserikali ilikuwa inaongozwa na chama gani, na sasa hivi ni chama gani kinaongoza?
 
Hivi kumbe mpaka leo kuna watu mnamuamini huyo mwehu? Poleni.
wapo wengi wakiwepo viongozi wako ndio maana baada ya yeye kutoa siri viongozi wako wamekimbilia kutoa utetezi. kama angekuwa haaminiki basi viongozi wako wangekaa kimya
 
wapo wengi wakiwepo viongozi wako ndio maana baada ya yeye kutoa siri viongozi wako wamekimbilia kutoa utetezi. kama angekuwa haaminiki basi viongozi wako wangekaa kimya
ATCL ni shirika la umma lazima litoe ufafanuzi kwa shutuma zozote dhidi yake na hawakumjibu huyo mwehu bali waliwatoa wasiwasi watanzania wapuuze huo uzushi.

Kwani ni mara ngapi taasisi za serikali zinatoa ufafanuzi juu ya habari za kughushi? Msigwa mara nyingi amekua akitoa kanusho kwa matamko fake yalioghushiwa kwa mfanano wa maelezo rasmi kutoka kurugenzi ya mawasiliano Ikulu.
 
Kama ni shuirika la umma kwanini lisubiri hadi mange kimambi atoboe siri na lemutuz atoe utetezi wa uongo ndipo nao waje kutoa utetezi?
 
kwanini lilisubiri hadi mange kimambi atoboe siri na lemutuz atoe utetezi wa uongo ndipo nao waje kutoa utetezi?
Kwa hiyo kila kitu kinachoendelea ATCL kitangazwe kwenye media? Huo utaratibu upo nchi gani? Watataarifiwa wahusika na sio kila mtu.
 
Kuna watu roho zinawauma wakiziona hizi ndege zinafanya vizuri, yaani wao leo wakisikia dreamliner imeanguka na kuua abiria wote inaonekana watafanya sherehe kubwa sana, upinzani wa aina hii upo Tanzania tu, mpinzani wa Nchi hii hana tofauti na gaidi
Gaidi ni yule anyeua watu na kuhihifadhi vikundi viohu vya wasiojulikan.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…