ATCL Imetangaza mabadiliko ya ratiba zake za safari za ndege

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,419
SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) leo tarehe 24 Agosti 2019 limetangaza mabadiliko ya ratiba zake za safari za ndege.

ATCL imetangaza mabadiliko hayo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, huku likieleza kwamba hatua hiyo inatokana na sababbu zilizo nje ya uwezo wake.

Hata hivyo, shirika hilo halijaweka wazi mabadiliko ya ratiba zake, na kuishia kuwaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza kwenye mipango yao ya safari.

“Wapendwa wateja wetu, kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wetu, Air Tanzania inasikitika kuwa taarifu kuwa kutakuwa na mbadiliko ya ratiba za ndege. Tuna waomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwenye ratiba/mipango ya safari zenu,” inaeleza taarifa ya ATCL.

Taarifa hiyo ya ATCL imekuja siku moja baada ya Mhandisi Isack Kamwelwe, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi kueleza kwamba ndege ya shirika hilo imezuiwa nchini Afrika Kusini kwa amri ya Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko Johannesburg nchini humo.

“Kwa mujibu wa taarifa ambazo serikali imepokea kutoka kwa balozi wetu nchini Afrika Kusini, ndege imezuiwa kwa amri ya mahakama. Serikali kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu inafuatilia suala hilo ili ndege hiyo iachiwe mara moja na kuendelea na safari zake kama kawaida,” amesema Mhandisi Kamwelwe.
Screenshot_20190824-144702.png
 
View attachment 1188993
serikali huwa hazifanyi biashara basi tu ya kwetu inajitoa ufahamu
 
Serikali kazi yake ni kuwekeza pale soko linaposhindwa, inaitwa Market failure... Na pia inawekeza kwenye miradi mikubwa ambayo soko haliwezi kuwekeza mfano kujenga mitambo ya kuzalisha umeme, reli nk...
 
hiyo sio biashara ni mazingira rafiki kwa watu wake kufanya biashara.
 
Dah kuna muda moyo wangu unauma kuona huyu mtoto bado hawezi kutembea.
 
safari chache tu SAA kaisoma namba mpaka wakakumbuka kuwa tunaweza kuzuia hii ndege kwa njia hii.
Baada ya SA, Tanzania ilitakiwa kuwa GIANT Kusini mwa jangwa la Sahara kiuchumi, kimaendeleo, kijeshi ila ni imekuwa ndivyo sivyo.
 
CEO kasema kuwa waliokata ticket watatafutiwa ndege zingine za mashirika mengine na kusafirishwa ila kwa sasa hawatapeleka ndege huko ila wataendelea katisha ticket
Hapo maana yake safari za SA zimefutwa kwa muda mpaka ufumbuzi wa kilichosababisha hio ndege ikamatwe upatikane.
 
Safari nyingine za ndani na nje zitakuwa impacted pia due to the missing aircraft.
 
Back
Top Bottom