Tunayo Shirika letu la Ndege la ATCL na sasa hivi kwa safari za humu nchini haina ushindani kabisa kwa lugha ya kimombo ina (monopoly). (1) Kwanza nianze na gharama zao mfano Mwanza mpaka Dar.
Gharama zao ni kubwa sana na kama ndege zilinunuliwa kwa ajili ya watanzania kwa nini sasa manufaa ya hizi ndege ni kwa matajiri tu?. (2) Huduma kwenye ndege zao haziridhishi kabisa.
Niwape mfano hai. Tarehe 17/9/2020 nilisafiri kwa ndege ya ATCL na muda wa kufika uwanjani nilielezwa ni saa 5.25 asubuhi. Nilifika muda muafaka na tukapaa saa 7.25 juu ya alama.
Kwa kawaida muda kama huo msafiri anatakiwa apewe chakula akiwa safarini hata angalau kinywaji lakini cha kushangaza tulipewa maji ya chupa ya ml.300 ikizingatiwa tulifika Dar es Salaam saa 9.45. Muda huu wote hatukupewa chochote.
Leo tarehe 23.9.2020 pia nimesafiri na ATCL na muda wa kufika kiwanjani ulikuwa saa 6.00 mchana na tumeondoka Dar kuja Mwanza saa 8.00 kamili juu ya alama. Tulitakiwa tuwe tumepatiwa chakula kama wasafiri lakini tuliambulia maji ya mil.300 aina ya Afya.
Leo nimeuliza hivi kwa nini hawatoi chakula kwa wasafiri, jibu nililopata eti ni kwa sababu ya corona. Nikawauliza hivi Ethiopian, Kenya Airways, Swiss Air hawatoi chakula kwa wasafiri kwa sababu ya corona?.
Wakanyamaza kimya. Kitendo wananchofanya ATCL kwa wasafiri ni kitendo cha kinyama na inabidi wabadilike.