ATCL kuanza huduma zake kesho

ATCL kuanza huduma zake kesho

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2009
Posts
5,471
Reaction score
752
Akijibu baadhi ya maswali ya wabunge juu ya kusimamishwa kufanya kazi kwa ndege za ATCL na lini zitaanza kazi, Ndemino, alisema taarifa alizonazo ndege hizo zitaanza kuruka tena kesho baada ya uongozi wa kampuni hiyo kupatiwa nyongeza ya Sh bilioni mbili na Wizara ya Fedha.


“Kwa taarifa zilizopo ni kwamba Sh bilioni mbili zinatarajiwa kutolewa leo (jana) na Hazina, zikishatolewa huduma zinaweza kuanza Ijumaa,” alisema Ndemino. Awali akijibu maswali ya wabunge wa kamati hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Magreth Munyagi, alisema kampuni hiyo ilinyang’anywa leseni yake ya kurusha ndege baada ya Shirika la Kimataifa la Ukaguzi wa Usafiri wa Anga (IOSA) kugundua dosari katika muundo na menejimenti, ndege, usafirishaji, matengenezo, chumba cha marubani, usimamizi wa mizigo na operesheni za kiusalama.


Alisema kutokana na kubadilishwa kwa kanuni za usalama ambazo zitaanza kutekelezwa Februari mwaka huu, TCAA ilitoa taarifa kwa kampuni zote za usafirishaji wa anga nchini zifanye marekebisho katika operesheni zake na kuyakabidhi kabla ya leseni zao kuisha muda.


Alisema hata hivyo ilipofika Desemba ndipo ukaguzi kutoka IOSA ulipoanza na TCAA iliamua kuchukua uamuzi wa kuinyang’anya leseni ATCL kwa vile ilikuwa bado haijakamilisha kwani iwapo IOSA wangegundua upungufu kwa kampuni moja ingeonekana Tanzania nzima ina upungufu.


Akisoma taarifa ya mamlaka hiyo, alisema moja ya changamoto kubwa zinazoikabili mamlaka hiyo ni ufunguaji wa soko kwenye sekta kwani Tanzania ni moja ya nchi zilizoingia mkataba wa soko huria kwenye usafiri wa anga hali ambayo itaongeza ushindani mkubwa kwa kampuni za usafiri wa ndege nchini.


Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohammed Missanga, alisema awali uongozi wa ATCL ulipatiwa na Serikali Sh bilioni 2.5 hali inayofanya mpaka sasa kampuni hiyo kupatiwa Sh bilioni 4.5 ili kukamilisha taratibu zake na ndege hiyo kuanza safari.


Aliitaka Mamlaka ya TCAA kuhakikisha kuwa inasimamia kampuni za ndege nchini katika suala zima la matengenezo ya ndege zao ili kuepusha ajali za mara kwa mara pamoja na kukatishwa safari hovyo hali ambayo inashusha kiwango cha huduma za ndege hizo.


Wabunge ambao ni wajumbe wa kamati waliouliza maswali kuhusu ATCL na majimbo yao katika mabano ni pamoja na, Suleiman Kumchaya (Lulindi), Paul Kimiti (Sumbawanga), Mtutura Mtutura(Tunduru), Ludovick Mwananzila (Kalambo) na Mbunge wa Rorya , Profesa Philemon Sarungi wote wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Back
Top Bottom