ATCL kujigamba kuhudumia wateja 60,000 kwa mwezi ni failure. Ni wazi kuwa ndege nane zilinunuliwa kwa cash bila kufanya tathimini yakinifu

huyo kenge hakujishughurisha kupiga hesabu ndogo kama hii, yeye anaona km abiria elf 60 kwa mwezi ni wachache
Abiria 60,000 ÷ ndege 8 = 7,500 kila ndege inabeba abiria 7,500 kwa mwezi.

7,500 ÷30 =250. Kila ndege inabeba abiria 250 kwa siku.
 
Nadhani wengi tunashupalia bila kuangalia kwa undani kuhusu operational cost za kuendesha hizi airline companies.
Watanzania wengi tunafuata mkumbo wa kisiasa bila kupata ukweli wa gharama na operation halisi za ndege. Kwa maoni yangu binafsi kwa nchi kama Tanzania ambapo ni moja ya kitovu cha utalii duniani ni vema kuwa na airline yake kama nchi, hii ina manufaa makubwa kuliko hasara. Japo jinsi ya kuzinunua hizi ndege ni mjadala mwingine ambapo kwa njia ya awali nakinzana nayo, siafiki kununua ndege hizi kwa cash, ila nakubaliana na Taifa kumiliki na kuendesha biashara ya ndege. Hii ni kwa manufaa mapana ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…