ATCL kupasua anga la India

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
552


HAYAWI hayawi sasa yamekuwa, baada ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL), kupewa kibali rasmi cha kuanza safari za ndege zake kwenda nchini India.

Akizungumza na Habarileo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladslaus Matindi alisema ni kweli wamepewa kibali cha kuanza safari za ndege zake nchini India, kilichotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usari wa Anga wa nchi hiyo.

“Tunashukuru, ni kweli tumepewa kibali cha ndege za ATCL kufanya safari nchini India, kibali kimetolewa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usari wa Anga wa nchi hiyo, kwa sasa hali ni hiyo ila taarifa zaidi tutazitoa baadaye,”alisema Matindi.

Miezi michache iliyopita, akizungumzia kuchelewa kuanza kwa safari hizo nje ya nchi, Matindi alisema ni kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, ikiwemo nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usari wa Anga (IATA).

“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usari wa Anga (IATA)ambayo kwetu kwa sasa tumeshakia mwisho,” alisema Matindi. Hata hivyo, ATCL kupitia kwenye mtandao wao yapata miezi kadhaa sasa, imekuwa ikitangaza bei za safari za ruti hiyo ya kwenda India katika jiji la Mumbai, ambapo wamesema bei ya kuanzia itakuwa dola 286 kwa daraja la kawaida na dola 455 kwa daraja la kwanza

Mapema mwaka huu akizungumzia ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner yenye uwezo wa kubeba abiria 282, ambayo ni moja ya ndege mpya zilizonunuliwa na serikali kwa lengo la kuboresha huduma za usari wa ndani na nje ya nchi, Matindi alisema ndege hiyo inaendelea na safari za ndani; na muda wowote kuanzia sasa watafanya uzinduzi wa safari za nje, ambako watazindua ruti ya kwenda Mumbai, India.

Akizungumzia safari za nje ya nchi, mwishoni mwa mwaka jana, Msemaji wa ATCL, Josephat Kagirwa alisema huo ni mpango mkakati wa ATCL wa miaka mitano, ulioanza mwaka 2017. Kagirwa alisema mkakati huo ni kuongeza huduma za usari wa ndege wa ndani na nje na kwamba mkakati huo utaboresha huduma za kampuni hiyo.

“Bei zetu kwa kuanzia ni zitakuwa dola 286 kwa safari ya kwenda au kurudi pekee, huku safari ya kwenda na kurudi itakuwa dola 455 za Marekani”, alisema Kagirwa. Akizungumzia kwa nini wataanza safari kwenda Mumbai, India, Kagirwa alisema wameangalia uhitaji wa soko, ambalo aliesema kwa utati waliofanya, kuna wateja wengi wanaotaka ruti ya moja kwa moja kwenda jiji hilo.

Alitaja sababu nyingine ni uhusiano wa muda mrefu baina ya India na Tanzania huku akisisitiza kuwa fursa za biashara, pia ni nyingi sambamba na wateja wanaokwenda kupata matibabu na elimu nchini humo. Kwa sasa ndege za ATCL zinafanya safari za kwenda Zambia, Zimbabwe na kwingineko, wakati maandalizi ya kuendea na safari nyingine za nje ya bara la Afrika ikiwemo Thailand, China na India kwa ndege ya Dreamliner na ndege nyingine mbili aina ya Airbus 220-300 yakiendelea.

Hadi sasa kampuni ya ATCL ina jumla ya ndege mpya sita, ambazo ni Bombadier Q 400 tatu, Boeing 787-8 Dreamliner moja , A220-300 mbili. Mwaka 1977 ATCL ilikuwa na ndege tisa, lakini kutokana na usimamizi mbaya kampuni hiyo ilishindwa kuendelea kutoa huduma za usari ipasavyo.

Mwaka 1994 iliunganisha nguvu na kampuni za ndege za Uganda na Afrika Kusini, ambapo zilifanya kazi kwa miaka sita hadi mwaka 2000, ilipotangaza kupata hasara ya Sh bilioni 50. Mwaka 2007serikali ililichukua shirika hilo lililoendelea kwa kusuasua.

Mwaka 2015 baada ya Rais John Magufuli kuingia madarakani, moja ya ahadi zake ilikuwa ni kununua ndege mpya, jambo alilotekeleza na hadi sasa zimeshanunuliwa sita.
 
Hongera ATCL nyumbu hawapendi habari nzuri kama hizi na hawawezi kucomment
Yap! Ni heri ya mego kavu pamoja na amani kuliko lilotoelewa pamoja na masimango!!

Mnaipeleka kwa wahindi hawa hawa waliogomea mbaazi zetu? Msije na pendekezo la air hostesses kuchangia gharama!!
 
Hiyo nauli ya USD 455 return trip ni ndogo kupita maelezo. Ilitakiwa angalau USD 1,000. Ni hasara.
 
wamebadili magoli

mwanzoni ilikuwa kuleta watalii

tukawauliza watalii wa Kihindi na Kichina?

sasa wanasema ruti hii ni mahitaji ya soko

wanatufanya Watanzania Wajingaaaa!
 
Reactions: BAK
Kwa kiswahili kilichoandikwa hapa,kama uandishi huu ulikuwa kwenye gazeti.Basi sarufi ya kiswahili inaposhwa kabisa
 
Tulikuwa na ndege 9 mpya za kisasa, tulishindwa. Leo tunazo 7, tunaamini tutafanikiwa kwa vile tu Rais ni Magufuli?

ATCL hawajatoa hata dola 1 kununua ndege, wamekodishiwa na serikali, lakini hasara bilioni 18.

Hata miaka 6 ijayo, kamwe ATCL hawataweza kutengeneza faida hata ya dola 1. Hatuyasemi haya kwa sababu ya kuichukia ATCL, serikali au Magufuli bali kutokana na ugumu wa biashara ya usafiri wa anga.
 
Watu kam wewe huwa siwapendi kabisa, sa kama hatuwezi ulitaka tufanye kitu gani. Maan hatukuwa na ndege mlisema hatuna ndege, tumenunua ndege mnasema hatuzihitaji, yaan kuongoza watanzania ni kazi Ngumu bora uwe kiongozi wa sokwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…