ATCL kupasua anga la India

wamebadili magoli

mwanzoni ilikuwa kuleta watalii

tukawauliza watalii wa Kihindi na Kichina?

sasa wanasema ruti hii ni mahitaji ya soko

wanatufanya Watanzania Wajingaaaa!

Ni kweli ni mahitaji ya soko.
 
Wasafiri wanajua faida ya direct flight. Ndege mpya tena. Dola elfu ni sawa kabisa
Ndege mpya au laa. Watu wanafata reputation ya shirika. Suppose uko India na ndege imepata techinical problem. Ndege.yenyewe moja, utarejea kwa ndege gani? Lakini shirika kama Emirates, QataR na Oman air watapeleka ndege nyengine ndani ya lisali.moja ishafika.
 

Haya makampuni kama Emirates hayana direct flight kati ya Dar na Mumbai. Inachosha sana kwenda kubadilisha ndege Dubai kwanza. Hasa kama ni mgonjwa au uko na mgonjwa.

Kwenye ndege yenyewe kuwa moja una point nzuri. Nadhani ikiharibikia huko basi watakodisha kutoka Air India au kampuni nyingine.

Safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja. Tutanunua nyingine zaidi.
 
Mkuu tatizo sio kununuwa au kuwa na ndege za ziada, tatizo ni uendeshaji mkuu! Ref mwendokasi.

Kama huniamini wachilia mbali unacceptable delays on domestic flights fanya utafiti wako wa ndege inayokwenda Comoro. Wiki iliyopita tu ndege inayokwenda Comoro wamewaweka watu siku 3 ndege haijaondoka. Kama una mgonjwa atafia airport kwa delays na hutopata hata atakayekwambia sorry japo unoficially. Trust me I love my country!
 

Yaani hata Jiwe ameweka watu wazembe kwenye ATCL? Mbona unanikatisha tamaa? Niko nje, sifuatilii mambo kwa karibu. Nilikua nimejiaminisha kwamba Jiwe hana mzaha.

Ila najua nauli ya kwenda India toka Tanzania ni dola elfu moja. Sasa hawa wanaosema dola 300 ni watu wa namna gani?
 
Usisikie maneno yao watu wachache kiongozi jpm kwel hana Mzaha ila kuna watu wafanya kila jitahida kumuangisha aonekane mbaya tu
 
Pole sana mkuu kwa kuwa underinformed. Jiwe sio Mungu wa kibaniani, hawezi kuwa everywhere with thousand hands. In reality, hatuna expertise ya kutosha kufanya biashara ya ndege, hii biashara ni kichaa. Nilwahi kuwemo kwenye hii industry kwa miaka 20, from Delta, AA, Qantas, nikamalizia na Gulf!
 

Nina swali kwenye hilo wazo lako kwamba hatuna utaalamu wa kutosha kuendesha shirika la ndege. Mbona kina nyie mpo? Mbona Precision walifanya tu vizuri mwanzoni? Kwani KQ na Ethiopian Airlines walianza wakiwa na utaalamu mwingi? Au Rwanda wametuzidi nini?

Nadhani tatizo ni mzizi wa ufisadi na uzembe uliojijenga miaka mingi.

Nikuchekeshe. Mwaka 1992 kulikuwa na ndege ta ATC ilikuwa inatoka Harare asubuhi kwenda Dar. Nilikuweko kwenye hiyo trip siku moja na wakatupa breakfast. Kulikuwa na vimkate vidogo kama sconces vilikuwa vinatoka Gloria Bakeries iliyokuwa Independence Drive (siku hizi Samora Machel). Walichonipa karibu kinivunje jino kilivyokuwa kigumu! Nikamwuliza Hostess vipi mbona kimkate jiwe hivyo? Akafoka "Kwani mimi ndiye mpishi hata uniulize?"

Wapo Watanzania wanaoweza kuendesha ATCL vizuri. Cha msingi viongozi wateuliwe through competitive processes na sio kwa upendeleo wa itikadi au kabila.
 

Precision kwa maoni yangu halkuwa nzuri service wise from the start, walinufaika na hela za kupiga tu za serikali. Unajuwa watu walikuwa hawasafiri lakini bado wanapewa receipt za tiketi, au watu kusafiri na kwenda holiday kwa pretence wanakwenda kwenye semina mkoa mmoja hadi mwengine.

KQ kama utakumbuka walianza chini ya uangalizi wa Wazungu. Ethiopia wao strategically ilibidi waanzishe shirika la ndege kwa ajili.ya usalama, kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa njia pekee ya kuaminika kiusafiri ni ndege kwa wakati huo. Na wakati huo nchi za Uarabuni bado zilikuwa zimelala. Rwanda Air usiitaje, inaendeshwa kisiasa tu na inalitia taifa hasara kubwa.

Hakuna Mtanzania, kwa mazingira ya sasa ya ATCL, anayeweza kuendesha hili shirika. Imagine ndege ina capacity ya abiria 72, abiria 68 on board tayari, wanaweza kuwa delayed kwa 2 hours kwa sababu hawa wanne ni maofisa wa serikali hawajamaliza mkutano. Shirika haliko independent. Hata huko Western countries mashirika yote yaliyokuwa yana mkono wa Serikali basi yamekufa kifo cha mende!
 
Dah kumbe ndivyo ilivyo.
Yaani watu 68 wanacheleweshwa kwa sababu ya watu 3 au 4.
Tanzania Bado sana ktk mambo haya.
Sasa kwa mfano Kama mtu una haraka let say umeitwa interview na unataka uende na kurud in the same day hawaoni Kama washakuvurugia.
 
Weeee ni mtoto Sana. Ndege za Mwl Nyerere alirithi toko EAC ndege nne . Mpya ni Boeing 737 mbili na zingine engne Moja toka Canada mbili. Jemba hili anazo tatu Q 400. A220.300 mbili na Boeing Moja kumbwa Hadi sasa. Anategemea kuwa na Boeing 787 nyingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…