ATCL kurejesha safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia Jumamosi, 22 Februari 2025

ATCL kurejesha safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia Jumamosi, 22 Februari 2025

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
590
Reaction score
807
SAFARI ZA IRINGA ZAREJEA, TWIGA MILES KUTUMIKA KUKATA TIKETI
122465390_f479262a-d9df-411a-98ea-c9abcd8ffae7.jpg

12 Februari, 2025, Dar es Salaam

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) inapenda kuujulisha Umma kuwa inarejesha safari za moja kwa moja kati ya Dar es Salaam na Iringa kuanzia Jumamosi, 22 Februari 2025.

Safari ya kwanza itaanza saa 3:00 asubuhi kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na itachukua takribani dakika 60 kufika Uwanja wa Ndege wa Iringa. ATCL itaanza na safari tatu kwa wiki; Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ikitumia ndege yake, DHC Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 6 katika Daraja la Biashara na 70 katika Daraja la Kawaida.

Nauli ya kwenda na kurudi ni TZS 199,200/= ikijumuisha mzigo wa hadi kilo 23, begi la mkononi lisilozidi kilo 7 pamoja na viburidisho ndani ya ndege bila malipo ya ziada. Aidha, Wanachama wa Twiga Miles wataweza kulipia tiketi kwa kutumia pointi zao, huku wasafiri wapya wakipata zawadi ya pointi 3,000 wanapojiandikisha kupitia Air Tanzania Mobile App.

Mteja ataweza kukata tiketi kupitia tovuti: www.airtanzania.co.tz, Aplikesheni ya Simu ya Air Tanzania, Kituo cha Huduma kwa Wateja (+255748773900) au Ofisi za ATCL.

Kurejeshwa kwa safari hizi kunalenga kuboresha muunganiko wa safari kwa wafanyabiashara, watalii, wakazi wa Iringa na wasafirishaji mizigo hivyo kufungua fursa zaidi za kibiashara na maendeleo katika mkoa huo na maeneo jirani.

Imetolewa na:

Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano kwa Umma
 
Back
Top Bottom