Atcl ndio naishia?

Fredrick Sanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2011
Posts
3,153
Reaction score
699
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]Tusijidanganye, ATCL siyo tena shirika la ndege[/TD]
[TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Wednesday, 11 April 2012 20:39[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

KUANGUKA kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Ndege wa Kigoma kumeliacha shirika hilo likiwa halina ndege hata moja inayofanya kazi, kwani ndege yake nyingine imekuwa katika matengenezo kwa muda mrefu sasa.

Hali hiyo bila shaka itakuwa imeifanya Serikali iukubali ukweli mchungu kwamba ATCL haikidhi tena vigezo vya kuwa shirika la ndege. Hivyo, tunadhani itakuwa imeona kwamba wakati sasa umefika wa kuacha porojo na kuanzisha shirika la ndege imara litakaloingia katika biashara ya ushindani na kupeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika anga za kimataifa.

Shirika hilo lilisema juzi kwamba ndege hiyo haifai tena kubeba abiria kutokana na kuharibika vibaya na kwamba halitatoa huduma za usafiri hadi hapo litakapopata ndege nyingine. Lakini katika hali ya kuonyesha kwamba moja ya matatizo yanayolikwaza shirika hilo ni ukosefu wa weledi kwa upande wa uongozi ni pale Kaimu Mtendaji wa shirika hilo, Paul Chizi aliposema juzi kwamba shirika hilo haliwezi kufa kwa kuwa lina mipango mingi ya kuhakikisha linafufuka.

Ni kweli kama alivyosema mkurugenzi huyo, ajali hiyo ya ndege hiyo ya ATCL imelisababishia shirika hilo hasara kubwa hata kama ilikuwa imekatiwa bima, kwani shirika hilo litalazimika kukodi ndege nyingine ili kuwasafirisha abiria ambao tayari walikuwa wamekata tiketi za kusafiri katika sehemu mbalimbali nchini. Jambo linalotupa wasiwasi ni pale tunapohisi kwamba shirika hilo linayachukulia kirahisi matatizo yanayolisibu hivi sasa kiasi cha kudhani kwamba, iwe isiwe litaendelea kuwapo.

Ndiyo maana hatuelewi wapi Kaimu Mkurugenzi huyo, Paul Chizi alikopata ujasiri alipowaambia waandishi wa habari juzi kwamba, shirika hilo linatarajia kupata mshirika wa kibiashara atakayekuwa anatoa huduma katika mikoa ya Mwanza na Kigoma. Tunasema hatujui alikopata ujasiri huo kwa sababu tukitilia maanani hali mbaya shirika hilo liliyomo, ni mwendawazimu pekee anayeweza kuwekeza au kujihusisha na shirika hilo kibiashara.

Tuliwahi kuonya kwamba ATCL haiwezi kuboresha huduma zake kwa wateja na kushindana katika soko la biashara hiyo ya usafiri wa anga kwa kauli za kisiasa kama anazotoa mkurugenzi huyo. Wakati alipoteuliwa kukaimu nafasi hiyo yapata mwaka mmoja uliopita, alitoa kauli zilizotafsiriwa kama kujipigia chapuo kwa lengo la kulinda ajira yake na wenzake, pale alipochukua muda mwingi kuishukuru Serikali kwa kufufua shirika hilo na kutoa ahadi tele kwamba shirika hilo lingefanya miujiza na maajabu, huku akijua kwamba shirika hilo halikuwa na nyenzo, mitaji wala rasilimali za kuliwezesha kutoa huduma kwa ufanisi.

Tulisema shirika hilo lisingeweza kufanya miujiza pasipo kupewa mtaji wa kutosha na pasipo kuwa na ndege zenye ubora, marubani na wahandisi wenye weledi na uzoefu wa kuliwezesha shirika hilo kuweka mazingira ya kushindana kibiashara. Tulisema pia Serikali ilipaswa kutoa dhamana ili liweze kupata mikopo ya kibenki. Mbona majuzi Serikali hiyohiyo iliidhamini Tanesco ili ipate mkopo wa Sh408 bilioni kutoka benki moja ya kigeni hapa nchini?

Tumesema hapo juu kwamba Serikali pengine itakuwa imeng'amua kwamba wakati wa maneno mengi na porojo umekwisha katika suala la uanzishwaji wa shirika la ndege lenye sifa na uwezo wa kupeperusha bendera ya nchi yetu kutokana na ukweli kwamba, ATCL ilianzishwa kuirithi ATC pasipo kuwapo dhamira, mipango na mikakati madhubuti ya kuingia katika soko la biashara ya ushindani ya usafiri wa anga.

Sasa tunaambiwa kuwa, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athuman Mfutakamba imelipa mamlaka shirika hilo mamlaka ya kukodi ndege kutoka mahali popote ili kuziba pengo lililoachwa na ndege ya shirika hilo iliyoanguka Kigoma juzi. Sisi tunadhani huko ni kukwepa tatizo, kwani ATCL ilivyo sasa haifufuliki. Serikali ijitose kwa kuanzisha shirika jipya na kulipatia mitaji ya kupata ndege za kutosha, watendaji wenye weledi na marubani na wahandisi wa ndege wenye uzoefu mkubwa.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

My Take: Hivi bado kuna haja ya kuling'ang'a, hili shirika wakati wazelendo wengine washaanzisha mashirika mengine? Ikibidi si Sirikali inunue hisa tu kwenye haya mashirika, kama Pressicion Air?
 
Tanzania nchi inayo ongozwa na porojo zaidi kuliko ualisia,waziri Nundu alikuja na porojo kibao,sijui zimeishia wapi!
 
Kwako mheshimiwa Nundu,

Naomba uzingatie haya ya msingi nayokuambia ukitaka ATCL ifufuke kwanza tunakuomba uwafukuze wote humo ndani including mkurugenzi wako Chizi. Pili ukamtafute Bwana Mwapachu na timu ya vijana wake waliotoka East African Airways waje kusaidia kuanzisha shirika hilo upya. Tatu timua bodi ya wakurugenzi yako na iweke ATCL katika interim supervision ya wizara. Nne wafukuze wafanyakazi wote wa ATCL na waajiriwe upya kama vibarua ili mpate nafasi ya kufanya assesment ya value ya ATCL na Mwisho kabisa mkishamaliza yote hayo na shirika likaanza kufanya kazi lipelekeni Dar-es-Salaam Stock Market liwe listed na serikali ibakiwe na 40% stake ya shirika.

Ikiwa yote hayo huyawezi nipe mie hilo shirika nitalifufua in 3 years but kwasharti kwanza sitaki wanasiasa waniingilie, pili nisiingiliwe katika maamuzi. Tatizo la ATCL ni management na wanasiasa mafisadi hakuna jengine. Haiwezekani we spend Billions of shillings katika ndege mtumba wakati ndege mpya Airbus ina cost just Bilioni 3 tu!!!! This is crazy.
 
Nadhani hatuhitaji kuwa na shirika la ndege la serikali

Mwanza



Kigoma




Hii nilikuwa najisikia fahari nayo sana kabla ya Mkapa na Mramba kuizika rasmi

 

Mdondoaji muache huyo ndugu yako Bakari Mwapachu ale pensheni yake kwa utulivu asije pata stroke bure uzeeni badala ya kupumzuka na kuangalia television; mikiki mikiki ya ushindani wa leo sio sawa na kukaa ofisini tuu na kuvuta cigar, dunia ya leo ni lazima mtu ajue kutwanga key-board ya huyo nduguyo mzee hajui; achana na kampeni yako hiyo humtendei haki huyo mzee.

Tatizo kubwa la ATCL ni kukosekana kwa commitment ya serikali kulifufua shirika; mwaka jana serikali iliahidi kulipa shirika shilingi bilioni 14 ili liweze kufufuka lakini cha kushangaza hizo pesa serikali mpaka hii ndege inaanguka huko Kigoma pesa shirika halikuwa limepewa!! Mpaka hivi sasa shirika halina bodi linaongozwa na Nundu mwenyewe contrary to laws of the land! Sasa namna hiyo hata akipewa malaika kuliongoza kweli shirika linaweza kufufuka?
 


Sijui kwa nini Watanzania wanataka kuwa na shirika la ndege linalomilikiwa na serikali. Kwa miaka mingi sana ATC na ATCL vimekuwa ni mzigo mkubwa kwa taifa. Ni muhimu tukubali kuwa serikali ya Tanzania haiwezi kabisa kuendesha biashara ya aina yeyote ile. Kuna kampuni ya ndege kama Cathay Pacific ilianzishwa na watu binafsi na leoo no kampuni ya tau kwa ukubwa duniani. Kwa nini sisi tunapenda serikali iwe ndiyo mmiliki? Mbona tulijitoa kwenye biashara ya kuendesha mabasi, malori na meli? Kwani kuendesha shirika la ndege ni rahisi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…