ATCL to write off the crashed plane!?

Bila shaka hiyo ndege (ambayo ni ya kukodi) ilikuwa na bima ama sivyo ATC wangeondolewa operating licence na kufutwa kwenye orodha ya IATA. Jambo kubwa hapa kama ilivyogusiwa na wengine ni kwa Serikali kuacha mzaha na kuamua kama kweli tuwe na shirika la ndege la umma au la. Utaona nchi kama Ethiopia ambao hawatufikii kiuchumi wamedhamiria kwa dhati kabisha kufanya biashara ya usafiri wa ndege - kwa kujituma na kujitolea hasa. Ni biashara ngumu sana na inayohitaji umakini na uzalendo wa hali ya juu kwelikweli. Hakuna mtu anayepewa nafasi ya kufanya hata chembe ya uhuni katika hilo - udhibiti ni zaidi ya asilimia 100.

Kwa uswahili tulionao sisi katika mambo yote ya msingi ni bora tukakaa kando na kuwakabidhi haki zetu za anga (freedoms of the air) wanaoweza kuifanya kazi hiyo nchini kwetu tukaambulia angalau royalties. Na tatizo letu kubwa hata tukileta wawekezaji/waendeshaji ama tunaishia kuambulia wababaishaji au tunawafanya hata walio makini waanze kukiuka viwango - kwa ajili tu ya kutaka pasenti holela na kupuuza udhibiti (regulation).
 
Well said Byasel. Kama mkataba wa ATCL na mkodishaji ulikuwa mzuri, basi ATCL wanatakiwa kupatiwa ndege nyingine ASAP au kulipwa fidia ya kukosa uzalishaji. Lakini hili hatujalisikia likinenwa pengine halipo.
 
Well said Byasel. Kama mkataba wa ATCL na mkodishaji ulikuwa mzuri, basi ATCL wanatakiwa kupatiwa ndege nyingine ASAP au kulipwa fidia ya kukosa uzalishaji. Lakini hili hatujalisikia likinenwa pengine halipo.

Maana kwa mawazo yako, ajali ilisababishwa na ubovu wa ndege au?
 
Injinia,
How will they bring it from Mwanza to Shaaban Robert Street?

Mh, good question S ni S. This Injinia had not thought about it.

Hmm....if only we had breakdown Landrover airplanes to tow it!!

I suppose they can disassemble it, as someone suggested. But that would take another year - mpaka iundiwe kamati ati!!
 
Mtazamaji,

Mimi na wewe tunaweza tukawa na mtazamo tofauti na Viongozi wa nchi kuhusu uwepo wa shirika hili. Lakini, ukimwuliza ghafla Mr. Presida au Mh. PM, atakuambia "...unajua Kenya wana shirika lao, Uganda wanalo, Rwanda wanalo, Msumbiji wanalo, Ethipoia wanalo; kwahiyo ni muhimu na sie tukawa na letu"
Ni STATUS tu hiyo, amini usiamini. Hakuna sababu nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…