ATCL tupieni macho kitengo chenu Cha Pacels(vifurushi) kwenda/kutoka Dar

ATCL tupieni macho kitengo chenu Cha Pacels(vifurushi) kwenda/kutoka Dar

Atclmzalendo

New Member
Joined
Oct 24, 2020
Posts
2
Reaction score
0
Ndugu wanajumuiya ya ATCL Kuna mapungufu makubwa kwenye upande wa kitengo kidogo Cha Parcels(vifurushi)kwenda mikoani,kwani wahusika siyo waaminifu kabisa asilimia kubwa ya mapato mengi yanaenda mifukoni mwa watu.

Kwa mfano:hapo nje departure karibu na sales office Kuna vijana madalali wa hizo parcels ambao wengi wao hawana hata vitambulisho vya TAA kazi yao ni kushawishi wafanyakazi kwa kuwapa 20000 mpaka 30000 inategemeana na ukubwa au uzito wa parcel yenyewe na wao kupeleka kwenye ndege kimagendo Bila kuwekewa tag yoyote,kwa hiyo parcel inaenda mwanza au mbeya bure bilakulipiwa huku wafanyakazi wenu wakitia hela mifukoni mwao.

Hapo nyuma kidogo Kuna binti aliajiliwa ATCL Kama office attendant Cha ajabu mkampeleka akahandle parcels alichokuwa anakifanya nikupiga hizo pesa Tena kijinga kabisa,waswahili wanasema ukila na kipofu usimshike mkono Sasa mwenyewe amekuwa mpaka akiwashika miguu,inasemekana Kuna watu wanamlinda office ya mjini na Airport,haiwezekani mtu aibe akatwe mshahara,Sheria za kazi ndivyo zinavyosema?

Mkurugenzi Kama hujui fuatilia hicho kitengo Cha parcels na mwisho ajirini watu kuendana na fani zao haiwezekani office attendant mkampe majukumu makubwa siyo hivyo tu huyo binti alishafukuzwa hata swissport kwa upigaji,
Mwisho nawatakia kazi njema ili shirika lifikie matarijio yaliyokusudiwa.
 
Tumia precision air wako vizuri kwenye parcel inasafiri kiofficiall ATCL hawana kifurushi cha percel sema wanafanya ujanja ujanja tu mfanyakazi anaenda nayo
 
Back
Top Bottom