Doctor Makunga
Member
- Jul 9, 2019
- 9
- 12
Ushauri kwa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuanzisha safari za kwenda kisiwa cha Mafia.
Kisiwa cha Mafia kina uwanja wa ndege ambao una uwezo wa kupokea ndege aina ya Fokker Friendship ambayo ATCL wanayo.Hivi sasa ndege zinazokwenda Mafia ni ndogo ambazo zinabeba abiria wachache na gharama zake zipo juu sana.
Mafia ni kisiwa chenye rasilimali za utalii na biashara ambapo kukiwa na ndege za uhakika shughuli za kibiashara na utalii zitashamiri katika kisiwa cha Mafia huku idadi kubwa ya abiria kwenda Mafia ikiongezeka.
ATCL wanaweza kuanzisha safari za ndege kwenda Mafia mara tatu kwa wiki kutoka Dar kwenda Mtwara kupita Mafia na kutoka Mtwara kwenda Dar kupita Mafia kama ilivyo kwa safari ya kutoka Dar kwenda Arusha kupitia Zanzibar zinazofanywa na baadhi ya mashirika ya ndege.
Route hii iwe ya jioni kwani itachochea kutumiwa na wafanya biashara wengi wanaoweza kwenda Mtwara asubuhi na jioni wakaondoka na ndege hii ya kupitia Mafia.
Route hii pia itaongeza watalii wa ndani watakaotembelea kisiwa cha Mafia kwa ajili ya holiday and leisure,beach resort,cultural tourisim,aidha wafanya biashara wataweza kupeleka bidhaa mbalimbali na kuchukua bidhaa Mafia kwa mfano samaki,prawns,nazi,n.k.Mzunguko wa fedha utakuwa na vipato vya watu wa Mafia vitaongezeka iwapo safari hizi zitaanza.Huu ni ushauri tu watu wa ATCL wafanye utafiti wa kina wakiona ipo tija wanaweza kuendelea nao wakiona hauna tija wataachana nao