BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
ATCL yaanzisha kibubu kwa abiria wanaotaka kulipia nauli kidogo kidogo
THURSDAY SEPTEMBER 09 2021
Summary
- Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeanzisha mpango wa "kibubu" utakaowawezesha wananchi kulipia kidogo kidogo mpaka atakapo kamilisha malipo ya tiketi yake ya ndege.
By Waandishi Wetu
More by this Author
Dar es Salaam. Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imeanzisha mpango wa "kibubu" utakaowawezesha wananchi kulipia kidogo kidogo mpaka atakapo kamilisha malipo ya tiketi yake ya ndege.
Katika mpango huo, mwananchi atatakiwa kuweka Sh50,000 kwa mara ya kwanza na kiasi kinachobakia atatakiwa kulipa kidogo kidogo kwa kiwango anachokimudu mpaka safari yake itakapofika.
Akizungumza na vyombo vya habari leo Septemba 9 jijini Dar es Salaam, mkuu wa kitengo cha mawasiliano - ATCL, Josephat Kagirwa amesema mpango huo utawawezesha wananchi kupangilia safari zao kwa kulipia tiketi zao kidogo kidogo.
Soma hapa: Kamati ya Bunge yang’aka deni, uendeshaji ATCL
"Tumeweka mpango huu ili kuwasaidia wananchi kuweka fedha kidogo kidogo ili kulipia tiketi ya ndege ndani ya muda ambao amepanga kusafiri," amesema Kagirwa.
Kwa upande wake, meneja wa mtandao wa safari na usimamizi wa mapato katika kampuni hiyo, Edward Nkwabi amesema kwa kuanzia wananchi watafanya malipo ya awali ya tiketi zao (booking) katika ofisi za ATCL lakini baadae wataweza kulipia kwa njia ya benki.
Amesema masharti yanayotumika katika mpango huo ni kama yale yale yanayotumika kwenye tiketi za kawaida. Amesema mteja akiahirisha safari yake, watazingatia vigezo na masharti kabla ya kumpangia safari nyingine.
"Shirika letu lina safari za ndege kila kona ya nchi hii na pia tunakwenda baadhi ya nchi kama vile Burundi. Kwa hiyo, mpango huu utatumika pia katika safari za kimataifa," amesema Nkwabi.
Soma hapa: Bosi wa zamani ATCL kulipa Sh8m au kwenda jela miaka minne
Naye Ofisa Masoko wa ATCL, Grace Magubo amesema kampuni hiyo itatoa zawadi kwa wateja ambao watahamasisha watu zaidi ya watano kutumia mpango huo wa kibubu na zawadi yao ni kujipatia tiketi ya ndege kwa nusu bei ya mahali anakotaka kwenda.
Imeandikwa na Peter Elias na William Bukoli.