ATCL yarejesha safari za Mtwara...

ATCL yarejesha safari za Mtwara...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801

WEDNESDAY, FEBRUARY 06, 2013

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) litaanza tena safari zake kati ya Dar es Salaam na Mtwara, kuanzia Ijumaa tarehe 8 February 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro alisema kuwa shirika lake litatumia ndege aina ya Dash 8-300 ambayo inauwezo wa kubeba abiria 50.

“Sasa tumejipanga upya kurejesha safari zetu kati ya Dar es Salaam na Mtwara ambazo zinatarajiwa kuanza Ijumaa, tarehe 8 mwezi huu wa Februari 2013. Urejeshwaji wa safari za kwenda Mtwara, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuongeza safari za kuenda mikoa mbali mbali ambayo tulikuwa hatuendi kwa sasa,” alisema.

Kapteni Lazaro alibainisha kuwa ratiba inaonyesha kuwa ATCL itaruka kwenda Mtwara katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili na kuongeza kuwa marekebisho ya ratiba yataendelea kufanywa kulingana na mahitaji ya wateja.

Alisema kuwa shirika lake litatoza nauli kuanzia shilingi 199,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi. “Abiria katika njia hii watahitajika kulipia kuanzia shilingi laki moja na tisini na tisa elfu kwa tiketi ya kwenda na kurudi. Abiria wanaweza kupiga simu namba 0782737730 ili wapate nafasi za usafiri. Vile vile abiria anaweza kupiga simu kwa mawakala walio karibu yao,” alisema.

Urejeshwaji wa safari za Mtwara unakuja mwezi mmoja baada ya shirika hilo kurejesha safari za Kigoma baada ya kumalizika kwa ukarabati wa uwanja wa Kigoma.

“Napenda niwahakikishie abiria wetu kuwa tutaendelea kutoa huduma bora kuliko zote kwa bei nafuu” alisema. Aidha, Kapteni Lazaro alisema kuwa shirika la ATCL lina mpango wa kuongeza ndege zaidi kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, na kubainisha kwamba wanategemea kuchukua ndege ambazo ni kubwa zaidi na za kisasa zaidi.

WEDNESDAY, FEBRUARY 06, 2013 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
 
Oh WOOW... Lakini Mr. CAPTAIN MBONA Hapo MBELE kwenye PICHA ya NDEGE ni AIRBUS?? Kwani TUNA AIRBUS??? SISI Tabia yetu si ni KUKOPA NDEGE MBOVU ziazopasuka VIOO???

Mara ya MWISHO TUMENUNUA NDEGE Kiwandani ni SERENGETI na KILIMANJARO Enzi za Mwl. NYERERE na alituma kina Captain MAZULA na AUGUSTINE MWINGIRA huko SEATTLE, WaSHINGTON!!!

*** Sasa HIVI TUNA PESA na MALI laini BORA kukimbiza USWISI halafu 10% na kuwapa wananchi NDEGE MBOVU za KUPANDA; nani analalamika??? Kila Mwananchi ANAIPENDA CCM DAMUUUUUUUUU...
 
Nasubiria kuona shirika la umma linalomikiwa na serikali kuweza kushindana kwenye the most competitive industry, mkiweza mimi kasheshe nitakuja ofisini kwenu kuwapongeza.
 
WEDNESDAY, FEBRUARY 06, 2013

SHIRIKA la Ndege la Air Tanzania (ATCL) litaanza tena safari zake kati ya Dar es Salaam na Mtwara, kuanzia Ijumaa tarehe 8 February 2013.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Kapteni Milton Lazaro alisema kuwa shirika lake litatumia ndege aina ya Dash 8-300 ambayo inauwezo wa kubeba abiria 50.

"Sasa tumejipanga upya kurejesha safari zetu kati ya Dar es Salaam na Mtwara ambazo zinatarajiwa kuanza Ijumaa, tarehe 8 mwezi huu wa Februari 2013. Urejeshwaji wa safari za kwenda Mtwara, ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wetu wa kuongeza safari za kuenda mikoa mbali mbali ambayo tulikuwa hatuendi kwa sasa," alisema.

Kapteni Lazaro alibainisha kuwa ratiba inaonyesha kuwa ATCL itaruka kwenda Mtwara katika siku za Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumapili na kuongeza kuwa marekebisho ya ratiba yataendelea kufanywa kulingana na mahitaji ya wateja.

Alisema kuwa shirika lake litatoza nauli kuanzia shilingi 199,000 kwa tiketi ya kwenda na kurudi. "Abiria katika njia hii watahitajika kulipia kuanzia shilingi laki moja na tisini na tisa elfu kwa tiketi ya kwenda na kurudi. Abiria wanaweza kupiga simu namba 0782737730 ili wapate nafasi za usafiri. Vile vile abiria anaweza kupiga simu kwa mawakala walio karibu yao," alisema.

Urejeshwaji wa safari za Mtwara unakuja mwezi mmoja baada ya shirika hilo kurejesha safari za Kigoma baada ya kumalizika kwa ukarabati wa uwanja wa Kigoma.

"Napenda niwahakikishie abiria wetu kuwa tutaendelea kutoa huduma bora kuliko zote kwa bei nafuu" alisema. Aidha, Kapteni Lazaro alisema kuwa shirika la ATCL lina mpango wa kuongeza ndege zaidi kabla ya mwishoni mwa mwaka huu, na kubainisha kwamba wanategemea kuchukua ndege ambazo ni kubwa zaidi na za kisasa zaidi.

WEDNESDAY, FEBRUARY 06, 2013 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG
anaongea kama kanywa mbege vile. eti bei nafuu! hivi hawaoni za fastjet? na wao wanaweza sema wanaoffer bei nafuu? ni waTZ wangapi wanaouwezo wakulipa sh laki 2 kasoro elfu moja? kama si mafisadi na wageni ndo watakaopanda hizo ndege.
watumalizie kujenga barabara yetu ya somanga sie walala hoi.
 
Yan majitu mengne kama malevi. hv wanadhan kw kufanya hvo ndo wataifunka fast jet? tatzo watanzania hatunaga blue prints
 
Yan majitu mengne kama malevi. hv wanadhan kw kufanya hvo ndo wataifunka fast jet? tatzo watanzania hatunaga blue prints

Mbona kama unajitukana mwenyewe? Mkuu kwani ATCL kuleta ndege ni kuwa wanataka kushindana na Fastjet? Au mwajiriwa wa Fastjet wewe? Be proud wewe kwa kampuni ya nyumbani, leo unaisifu Fastjet ngoja ikutie cost ndo utaona. Usije ukaja ukalalamika kuwa service mbovu za fastjet, be prepared, you get what you paid for!

ATCL hongereni! Mambo kidogo kidogo, hebu tuwe na upendo kwa shirika letu, aibu TZ tunashindwa kuwa na ndege, wenzetu KQ wako mbali, coz ya uzalendo.
 
Back
Top Bottom