ATCL yasitisha safari za ndege Afrika Kusini - wadai sababu vurugu

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Asha Bani, Dar es Salaam

Siku moja baada ya Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), iliyokuwa inashikiliwa kwa amri ya Mahakama ya Gauteng nchini Afrika Kusini, kabla ya mahakama hiyo hiyo kuamuru iachiwe jana, imewasili nchini huku ikisitisha safari zake nchini humo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Septemba 5, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe ndege hiyo imetua nchini jana saa moja usiku lakini itasitisha safari zake za kwenda Afrika Kusini kwa sasa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo vurugu zinazoendelea nchini humo.

β€œSababu hizo ni pamoja na usalama wa chombo chenyewe kutokana na hali ya vurugu iliyopo nchini humo hadi pale tutakapohakikishiwa usalama wetu na abiria.

β€œWanasheria wamebaki Afrika Kusini wakiendelea kufuatilia hukumu iliyotolewa na kuhakikisha aliyefungua kesi analipa gharama zote,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, amesema leo asubuhi ndege hiyo imefanyiwa ukaguzi iko salama inasubiri kupangiwa safari ya njia nyingine itakayoanza leo saa tisa alasiri.

 
Uncle Tom (Tony254) ulikuwa ukituhasa kwamba dawa ya deni ni kulipa, dawa ya deni ni sheria tu sio kulipa hovyo kipimbi, kibabu chenu lazima kilipe hasara yote tulioipata

Hehehe!! Mumeikimbia SA wale 'comred' wenu wa damu mliowakomboa kisa babu mzungu, dawa ya deni ni kulipa, la sivyo mzipigishe ruti za ndani ya Bongo, maana huko nje zitakamatwa hadi mkome, kumbuka Canada alishakwapua cha kwake mapema, wengine wanaowadai walikua wameanza kuzisubiri, hii ni kutokana na majigambo yenu ya kudai mlizinunua kwa pesa ya ndani.
Yaani una madeni chungu nzima halafu unajidai umenunua madubwasha kwa hela ya ndani......
Ukiwa maskini kubali umaskni halafu uufanyie kazi, wacha kutunisha misuli walipo mabwana wakuu maana utaondolewa kwa vibao.
 
ha ha jana jamaa kaanzisha thread eti "TZ NI KALI", kama ninyi ni wakali si mngeendelea na safari za SA,
wacheni kusema ni violence, unataka kusema Kibera kukiwa na violence Emirates au Ethiopian airlines zitasimamisha safari zake kutua JKIA??? ... WACHENI UJINGA.... πŸ˜› πŸ˜› πŸ˜›
 
Wa kutuambia Tanzania tuna madeni
 

Attachments

  • D9YLS2qXsAAehEs.png
    26.3 KB · Views: 18
Tumewawekea vikwazo wa usafiri wetu hatuwapelekei watumie hiyo mingine inayo gharimu pesa nyingi tunawapelekea wengine huduma SA yupo kwenye vikwazo afaidi matunda ya ATCL
 
Deni lenu hata EAC member states wote kwa ujumla hatulifikii, mna madeni mpaka matakoni na tumenyamaza πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Deni lenu hata EAC member states wote kwa ujumla hatulifikii, mna madeni mpaka matakoni na tumenyamaza πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hamuwezi mkafikia maana nyie ni maskini hamkopesheki, na kidogo mnachokopeshwa inabidi mali zenu zishikiliwe kwa mlivyo wazembe wa kulipa.
Aibu ndege mbili zimekamatwa hadi sasa, hasara yote hiyo ndege imeegeshwa siku zote hizo ambapo ilikua inafaa kuwa angani inapiga misele. Sasa kwa uwoga wa kulipa madeni imebidi msitishe safari zote za kwenda kwa 'comred' wenu mliomwaga damu kuwakomboa, maana inawezekana huyo mkulima ni mmojawapo wa wakulima na wafanyi biashara wengine wengi wanaozisubiri.
Nyie mna gundu aki ya nani, huku ndege bado halijatua kule Total amechomoa bomba
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Na mbona your debt to GDP ratio ipo kubwa zaidi ya wazembe?

Incase you don't know what is it ni kwamba a high ratio means a country isn't producing enough to pay off its debts

Maana yake ninyi wavivu na masikini
 
Alafu anasema hatukopesheki, mbona ni wao juzi kati walinyimwa loan [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Alafu anasema hatukopesheki, mbona ni wao juzi kati walinyimwa loan [emoji23][emoji23][emoji23]
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Kenya imefika hatua ya Kukopa pesa ya kulipa mkopo, wameparara hata pesa ya kulipa wafanyakazi hawana, serikali imepiga marufuku kuajiri mpaka miaka 6 ijayo
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Na mbona your debt to GDP ratio ipo kubwa zaidi ya wazembe?

Incase you don't know what is it ni kwamba a high ratio means a country isn't producing enough to pay off its debts

Maana yake ninyi wavivu na masikini

Debt to GDP ratio ya Japan ni 222% lakini hao Japan wanawazidi nyie kiuchumi mara zaidi ya mia, na ni mojawapo wa mataifa yanayowapa misaada, ukikumbuka hata flyover mnayopenda kwenda kupigia mapicha hapo wao wamewajengea kama msaada.
Hivyo hicho sio kigezo cha kuangalia, cha msingi ni nchi inazalisha vipi kiuchumi. Unaweza ukawa na uwiano mkubwa lakini bado unakopesheka maana ukifanyiwa tathmini unaonekana kuwa shwari kiuchumi, lakini pia uwiano unaweza ukawa mdogo ila wewe tayari mifupa hapo ulipo. Leo hii mwarabu wa Oysterbay au huko Mikocheni ambao humiliki uchumi wa Tanzania akiingia kwa benki kuomba mikopo, atapewa hata kama analo deni, maana ana nafuu, laakini kajamba kama wewe wa Tandale unayeishi kwa buku saba za Lumumba hata kama haudaiwi na mama nitilie, hupewi hata shilingi maana tayari wewe mwenyewe hoi full mifupa.
Hadi hapo ndege mbili zenu zimekamatwa mumeshindwa kulipa madeni ya watu, zichomoeni tena kwenda South zinasubiriwa na wakulima, utakuta labda hata kuna mliowadhulumu kwenye migodini.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23] Kenya imefika hatua ya Kukopa pesa ya kulipa mkopo, wameparara hata pesa ya kulipa wafanyakazi hawana, serikali imepiga marufuku kuajiri mpaka miaka 6 ijayo
 
Tulishawaambia hawa jamaa kuwa ndege inarudi...
Naona sasaivi ni kama tunamdai sisi.

Reputation damage, Flight cancellation cost, Gov disturbances, crew living costs, Crew disturbances, Tanzania delegates and Lawyers costs, plus many more.......


Pumbavu sana
 
Watu walipe deni wakue free kuenda popote duniani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…