#COVID19 Atembea kwa miguu kutoka Kigoma hadi Kilimanjaro kuhamasisha chanjo

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imemtambua Mwanariadha Michael Filberth Nondo, mkazi wa Kigoma aliyejitolea kutembea kutoka mkoani Kigoma mpaka mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuhusu ugonjwa wa UVIKO-19 na kuchanja Chanjo dhidi ya Uviko -19.

Katibu Mkuu Wizara ya ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Prof. Abel Makubi, ameueleza Umma kupitia Vyombo vya Habari akimwakilisha Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima jijini Dodoma.

“Kama Serikali tunatambua juhudi zinazofanywa na wadau mbali mbali katika Mapambano haya ya Corona, lakini kwa leo kama Wizara niseme, tumetambua ndugu Michael Nondo, aliye onesha Ujasiri na Uzalendo wakutembea kutoka mkoani Kigoma mpaka mkoani Kilimanjaro ikiwa ni sehemu yakuunga Mkono juhudi zinazo endelea nchini kote.” Amesema Prof. Makubi.

Kwa kutambua Mchango wake, Prof. Makubi amemkabidhi Cheti na kumpa hadhi ya ukamanda wa Kuhamasisha Wananchi kupata Chanjo kwa kuthamini mchango na uzalendo wake katika kampeni hiyo ya uchanjaji.

Kwa upande wake, mwanariadha huyo amesema, sababu kubwa iliyo msukuma kufanya zoezi hilo ni imani aliyonayo juu ya serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na sekta zote ikiwemo sekta ya Afya katika Mapambano dhidi ya Uviko- 19.

Hii ni mara ya pili kwa Nondo, kufanya safari hiyo baada ya kufanya zoezi kama hilo mwezi wa sita Mwaka huu kwa mara ya kwanza, kisha kujipumzisha kwa miezi miwili kabla ya kurudia tena awamu hii,

“Mara ya kwanza kufanya safari hii nilikuwa nikifanya usiku lakini hivi sasa nimeamua kufanya mchana ili kila mmoja anione, ninawashukuru sana Serikali hususan ngazi za Serikali za mitaa nilipoweza kupita ambapo walinipa sehemu za kulala na kunikutanisha na wananchi, kunitambulisha na kuongea nao kwa lengo la kutoa Elimu juu ya ugonjwa huu” amesema Nondo

Ametoa wito kwa vijana, watu wa makamo na wazee kwenda kupata chanjo kwa hiari kwa sababu chanjo hiyo haina madhara na kushauri kuacha kusikiliza tetesi zisizokuwa za kweli na zenye lengo la kupotosha.

Amewataka watanzania wajue kuwa Taifa linawahitaji kwaajili ya kujenga Taifa hivyo kujitokeza kupata Chanjo pamoja na kuchukua tahadhari za Maradhi ikiwepo UVIKO-19 ni muhimu sana kwao.

IMG-20210926-WA0051.jpg

IMG-20210926-WA0048.jpg

IMG-20210926-WA0043.jpg
 
Kuna mwingine huko sijui Tunduru ambaye ni afisa afya yeye anazunguka nyumba kwa nyumba kuchoma watu chanjo.
👇🏾
IMG_20210927_091748.jpg

Na inasemekana amefanikiwa kuchoma watu kadhaa na wakati huo huo tunaambiwa hiyo chanjo inaweza kuhifadhiwa kwenye jokofu kati ya 2° C na 8° C (36° F na 46° F) mpaka mwezi 1 (siku 31). Baada ya siku 31 inasemekana haifai kwa matumizi.

Na kwa hali hiyo wataalamu au watengenezaji wake wanasema haiwezi kukaa nje ya jokofu kwa 12hrs, sasa huku kwetu mtu anazurula na kile kibox hata hajui thamani ya matumizi.
 
Kuna mwingine huko sijui Tunduru ambaye ni afisa afya yeye anazunguka nyumba kwa nyumba kuchoma watu chanjo.
👇🏾
View attachment 1954365

Ila wabongo kwa ubishi hamjambo halafu mnajifanya mnajua kila kitu yaani.

Na kibaya zaidi hamuulizi kwa kutaka kujua, mnauliza kwa kutaka kubishana.

Janssen ( J&J ) inahifadhiwa ndani ya joto la +2 mpaka +8C ila ikitokea kuna huduma za Mkoba inatakiwa chanjo ibebwe kwenye kibebeo maalum cha chanjo ( Vaccine carrier ) ambacho ndani yake unapaswa kuweka cool water ice packs ).

Pia unapaswa kuepuka direct sunlight. Hii ni kwasababu huwezi kutembea na jokofu la chanjo kwenye outreach.

Na suala la kuexpiry baada ya kukaa kwenye Jokofu siyo siku 31 bali ni miezi 3.
 
Ahsante kuwasaidia wajinga, wabishi bila kutaka kujua ukweli!
 
mpeleke haraka kwa Gwajima akaombewe huyo ...
 
Ila wabongo kwa ubishi hamjambo halafu mnajifanya mnajua kila kitu yaani.

Na kibaya zaidi hamuulizi kwa kutaka kujua, mnauliza kwa kutaka kubishana.

Janssen ( J&J ) inahifadhiwa ndani ya joto la +2 mpaka +8C ila ikitokea kuna huduma za Mkoba inatakiwa chanjo ibebwe kwenye kibebeo maalum cha chanjo ( Vaccine carrier ) ambacho ndani yake unapaswa kuweka cool water ice packs ).

Pia unapaswa kuepuka direct sunlight. Hii ni kwasababu huwezi kutembea na jokofu la chanjo kwenye outreach.

Na suala la kuexpiry baada ya kukaa kwenye Jokofu siyo siku 31 bali ni miezi 3.
Sijui akili huwa zinakwenda mapumzikoni, nani alikuwa anabishana na nani mbona unaleta ujinga kwa wenye akili!.
 
Attachments

Sema hutaki, wacha kutia sumu wenzio. Ni ujinga mkubwa kukataa chanjo! Shame on you!
Pia ni ujinga mkubwa sana kukubali chanjo acha kupotosha umma kuaminisha kwamba chanjo ni salama...mbona hamjaleta chanjo ya ukimwi haraka hivyo....unatetea biashara za watu,wenzako wanakula faida tu.
 
Nenda shule kwanza maana hujui hata chochote kuhusu chanjo, la sivyo usingelinganisha korona na ukimwi! Kweli Magufuli alihamisha akili zenu, akaenda nazo nanyi mkakubali na kubaki na ujinga wake! Shame!
 
Mambo mengine ni ya kujitesa tu. Binafsi siwezi kufanya upuuzi kama huo.
Mpaka Sasa Hivi Serikali Imefarakana Kuhusu Chanjo
Kuna Hawa Kabudi Msukuma Jafo Na Wengine Kimya
hawasemi Lolote Nao Wamebaki Midomo Wazi
 
Kuna mwingine huko sijui Tunduru ambaye ni afisa afya yeye anazunguka nyumba kwa nyumba kuchoma watu chanjo.
👇🏾
View attachment 1954365

Na inasemekana amefanikiwa kuchoma watu kadhaa na wakati huo huo tunaambiwa hiyo chanjo inaweza kuhifadhiwa kwenye jokofu kati ya 2° C na 8° C (36° F na 46° F) mpaka mwezi 1 (siku 31). Baada ya siku 31 inasemekana haifai kwa matumizi.

Na kwa hali hiyo wataalamu au watengenezaji wake wanasema haiwezi kukaa nje ya jokofu kwa 12hrs, sasa huku kwetu mtu anazurula na kile kibox hata hajui thamani ya matumizi.
Haa Haa Haa Haa Haa Haa
Wazurura Na Chanjo
 
Nenda shule kwanza maana hujui hata chochote kuhusu chanjo, la sivyo usingelinganisha korona na ukimwi! Kweli Magufuli alihamisha akili zenu, akaenda nazo nanyi mkakubali na kubaki na ujinga wake! Shame!
Virusi vya ukimwi
Virusi vya corona
Hiyo shule yako inasemaje....chanjo ya virusi vya corona imepatikana...lakini ya virusi vya ukimwi?
Piga kampeni makampuni yaingize pesa kijana.
 
Back
Top Bottom