Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
ATHARI YA MAJINA YA MITAA KATIKA HISTORIA YA TANGANYIKA
Mtaa wa Makunganya unaanza karibu ya Msikiti wa Shia ambao uko kwenye kona ya Mtaa wa Zanaki unashuka chini kama unakwenda Picha ya Bismini (Askari Monument) na kabla ya kufika Picha ya Bismini inapita pembeni ya Msikiti wa Ngazija na kukutana na Mtaa wa Mkwepu hatua chache kutoka hapo.
Huyu Makunganya jina lake kamili ni Hassan bin Omar Makunganya.
Hassan Omar Makunganya alinyanyua silaha dhidi ya Wajerumani na ana historia ya kutukuka katika kupinga utawala wa Wajerumani.
Alipokamatwa alikutwa ana nyaraka zake binafsi nyingi ambazo zinaeleza mengi katika yale yaliyokuwapo wakati ule wa mapambano na adui aliyevamia nchi yake.
Nyaraka hizi kaandika Hassan bin Omar Makunganya mwenyewe kwa mkono wake kwa hati za Kiarabu.
Wajerumani waitumia nyaraka hizi mahakamani kama ushahidi wa kuthibitisha ‘’uhaini,’’ wa Hassan bin Omar Makunganya dhidi ya serikali.
Kutokana na ushahidi huu Hassan in Omar Makunganya alinyongwa Kilwa.
Nyaraka hizi utazipata Zentrum Moderner Orient (ZMO), Berlin.
Hassan bin Omar Makunganya jina lake limewekwa la kwanza katika Mnara wa Kumbukumbu ya Vita Vya Maji Maji ingawa yeye wakati wa vita hivi alikuwa tayari keshanyongwa.
Hassan bin Omar Makunganya alinyongwa mwaka wa 1895.
Kumbukumbu ya Hassan bin Omar Makunganya ni huu mtaa uliopewa jina lake hapa Dar es Salaam.
Laiti mtaa huu ungeandikwa kwa jina lake kamili ungeitwa, ‘’Mtaa wa Hassan Omar Makunganya.’’
Mtaa wa Mkwepu ambao unakatiza mtaa wa Makunganya ni kwa heshima ya Rashid Mohamed Mkwepu.
Mtaa wa Makunganya unakwenda na kuishia Picha ya Bismini na mbele ya picha hii ni Mtaa wa Samora Avenue.
Rashid Mohamed Mkwepu alikuwa mmoja wa wanachama wa mwanzo wa TANU na mtu aliyekuwa karibu sana na Julius Nyerere wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika lakini alijulikana kwa jina lake la utani la ‘’Sisso.’’
Kama alivyokuwa Hassan bin Omar Makunganya na Ali Msham katika historia ya Tanganyika, Rashid Sisso alikuwa mtu wa Kilwa.
Huu Mtaa wa Makunganya unapokutana na Mtaa wa Mkwepu, mtaa huu unakwenda hadi unakutana na Mtaa wa Zanaki na Mtaa wa Mkwepu ulipo Msikiti wa Bohara.
Hapo unaanza Mtaa wa Kaluta unaoishia Barabara ya Morogoro.
Si wengi wanaoijua historia ya Kaluta.
Kaluta alikuwa mmoja wa wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Jina lake kamili ni Kaluta Amri Abeid na alisoma darasa moja na Julius Nyerere Tabora School.
Ile namba moja katika mtihani pale Tabora School walikuwa wakipokezana Kaluta Amri Abeid na Julius Kambarage Nyerere.
Mitaa hii yenye majina ya wazalendo wa Tanganyika ingeandikwa majina kamili ya wazalendo hawa athar yake ingekuwa kubwa katika jamii na ingesaidia sana katika kujua historia ya Tanganyika.
Picha: Kulia Hassan bin Omari Makunganya, Omari Muenda na Jumbe (1895).
Kushoto Hastings Kamuzu Banda, Julius Kambarage Nyerere, Rashid Mohamed Mkwepu na Kaluta Amri Abeid (1950s).