Athari ya vita duniani na hali ngumu ya uchumi sasa na baadaye. Nini kifanyike?

Athari ya vita duniani na hali ngumu ya uchumi sasa na baadaye. Nini kifanyike?

mwanamichakato

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
1,188
Reaction score
1,090
Kutokana na sababu mbalimbali Hali ya uchumi wetu yamkini si nzuri sana hivyo hata Kama haisemwi lakini kuna mambo yanaakisi hili.Kama taifa yatupasa kushikamana sana na kuhamasisha uzalishaji wa ndani Kwa Kiwango kikubwa ili kuondoa utegemezi wa bidhaa toka nje na matumizi makubwa ya fedha Za kigeni..

Jitihada nyingi sana zinafanywa na serikali yetu kuhakikisha mambo yanatengemaa na tupaswa kuendelea kuwaombea hekima na maarifa viongozi wetu..Vivo hivyo si dhambi kushauri inapobidi.

Nchi nyingi Za dunia ya tatu zinaguswa moja kwa moja na vita na kukosekana Kwa Amani duniani kote..Hasa Urusi vs Western Powers (Ukraine), Israel vs Hamas/Hezbollah; Houthi (Yemen) vs ..; Chokochoko Za Korea ya Kaskazini dhidi korea/Japan n.k. West Africa instability na mivutano kati ya Uchina na Marekani juu ya Taiwan..

Ama Kwa hakika hatupo salama sana sababu matumizi makubwa ya fedha yameelekezwa ktk migogoro ya kivita hivyo kuathiri biashara ya dunia na Amani Kwa ujumla..Uchumi wetu si wa viwanda,Uvuvi wala kilimo Bali uchuuzi Kwa sehemu kubwa..Tunapata shida. Mathalani leo Dola ipo juu na Haipatikani na wakati huo kusafirisha kasha la futi 40 ni takribani Usd 7700 toka Uchina mpaka Dar es salaam toka dola 3300 —4200 ..miezi michache ijayo tutegemee bidhaa kupanda..

🌸Viwanda vichache tulivyonavyo vinaathirika sababu ya kutegemea malighafi/vipuri toka nje,Wafanyabiashara wa kati na wadogo wanaathirika na mdororo wa uchumi..Hali kadharika watumiaji wa mwisho nao Wapo ktk kipindi kigumu Kwa namna moja au nyingine..

🌸Tutegemee kodi Za ndani,forodha na nyinginezo kupungua sana ndani ya miezi sita mpaka 12 ijayo..Vivo hivyo taasisi Za fedha yamkini zikapata changamoto kubwa ya deposits na NPL..Na pia Upo uwezekano wa biashara nyingi kujinyonga..

🌸Ushauri:Serikali ipunguze matumizi yasio ya lazima..Vikao,Warsha,Sherehe,Matamasha,Makongamano,Shamrashamra,Maadhimisho..

🌸Bunge Lipinguzwe ukubwa Kwa kuunganisha baadhi ya majimbo;Viti maalumu viondolewe.

🌸Mishahara ya wabunge,Mawaziri,Manaibu Mawaziri na Wakuu wa Mikima ipunguzwe Kwa asilimia 40..

🌸Ruzuku Za vyama Vyote vya siasa zifutwe..

🌸Baraza la Mawaziri Lipunguzwe ikibidi Kwa nusu ya idadi.
 
Ruzuku ifutwe ili vyama vya upinzani vife?

Ccm wenyewe hawana shida na Ruzuku kwa sababu Hazina yote ya Nchi iko mikononi mwao 👁🙄

Labda ungesema Ccm wasipewe ruzuku maana hata hivyo pamoja na kuwa Serikali ni yao na pia Ruzuku huwa wanapewa pesa nyingi sana sana kuliko wenzao. 👁🙄

Muwe na Huruma basi hata kidogo,
Hii Nchi ni yetu sote 😳👁
 
Athari za vita huwa hazichagui dini wala kabila tena watu wa Dunia ya tatu ndio tutaingia kwenye matatizo makubwa ya kiuchumi!
 
Mi naona chanzo cha matatizo makubwa ni kumwekea vikwazo yule mbabe wa kaskazini mashariki. Tofauti na hapo mambo yalikuwa simple kabisa
 
Back
Top Bottom