Hilary Nyengela
New Member
- Jul 13, 2022
- 2
- 2
ATHARI ZA BARIDI KALI KATIKA MKOA WA NJOMBE. Habari,nawasalimu wote kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkoa wa Njombe upo ukanda wa nyanda za juu kusini,latitudo ya 08'50" na 10'30" kusini mwa ikweta pia mashariki mwa Greenwich upo katikati ya longitude ya 33'45" na 35'45",ukiwa na ukubwa wa mita za mraba zipatazo 24,994,ambapo 21,172km ni nchikavu na 3,822km zimetawaliwa na maji.
Umbali upatao 2,200km za mraba kutoka usawa wa bahari zinapelekea mkoa huu kuwa na baridi kali hasa majira ya mwezi wa tano mpaka wa nane.
Hivyo basi kutokana na uwepo wa baridi kali katika mkuu huu kiujumla umenipelekea kuandaa makala hii itakayoeleza athari za baridi kali kwa Wananchi waishio mkoani humu.
Kudorora kwa ufaulu wa kimasomo kutokana na mahudhurio duni.
Kupata magonjwa kama vile mafua makali,kikohozi, vichomi na homa za mara kwa mara,pia magonjwa ya ngozi na mba.
Kuchochea umasikini kwa kiasi kikubwa kwani kipato cha Wananchi kinategemea kazi za kila siku,uwepo wa baridi unachochea uvivu kwa kiasi kikubwa.
Kuzorota kwa shughuli za kijamii na kiuchumi kama vile kilimo na hivyo kudumaza uchumi wa taifa letu.
Licha ya Mkoa huu kubarikiwa kuwa na rasilimali nyingi na utajiri wa kutosha, kama athari za baridi kali zisipochukuliwa hatua zinaweza kupelekea madhara haswa kwa Wakazi wa Njombe na taifa kwa ujumla.
Hivyo basi ni vyema kwa mamlaka husika kuweza kuainisha changamoto kutokana na baridi kali katika mkoa wa njombe. Mbinu zifuatazo zinaweza kusaidia katika kuleta chachu ya maendeleo; Uvaaji wa suruali ndefu, kofia, viatu na makoti mazito ili kujilinda na baridi.
Uboreshaji wa miundombinu ya shule kama vile madirisha na dari ili kuzuia baridi.
Uwepo wa uji kwa wanafunzi wa shule haswa watoto wadogo ili kujikinga na baridi kali.
Ni matumaini yangu andiko hili litasaidia kuleta mabadiliko chanya sio tu mkoani Njombe bali hata mikoa ya jirani inayokubwa na baridi kali.
Nashukuru kwa nyote mliosoma makala hii matumaini yetu kwamba kutakuwepo na mabadiliko makubwa ili kuweza kuokoa kizazi kijacho kinachopotea kwa athari za baridi mkoani Njombe.

Upvote
5