Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Australia imekumbwa na mporomoko mbaya zaidi wa uchumi katika robo ya kwanza tangu kutokea kwa mdorororo mkubwa kabisa wa kiuchumi duniani wa miaka ya 1930. Hali hiyo inatokana na janga la virusi vya corona, ambapo data zilizotolewa leo zinathibitisha kuwa nchi hiyo inakabiliwa na mdororo wake wa kwanza katika kipindi cha miaka 28.
Rekodi za kitaifa zinaonesha uchumi umesinyaa kwa asilimia 7 katika mwezi wa Juni, kikiwa kiwango kikubwa cha kupungua tangu kuanza ukusanyaji wa data hizo mwaka 1959. Kiwango cha mporomoko kilichorekodiwa kufanana na hicho kilikuwa cha asilimia 2 kwa Juni 1974, ambapo wachumi wanakadiria kuwa uporomokaji mkali ulitokea mapema katika miaka ya 1930, pale ambapo Australia lilipokuwa moja kati ya mataifa yalioathiriwa vibaya zaidi na mproromoko wa uchumi wa kihistoria ulioikumbwa dunia.