JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Afya ya akili huchangia moja kwa moja katika uwezo wa kuzalisha wa binadamu yeyote, ubora wa mahusiano na pia kiasi cha kufurahia maisha. Afya ya akili huchochewa na factors za kibaiolojia, kisaikolojia, kijamii na kihisia.
Ingawa Siku ya Dunia ya Afya ya Akili imeanza kusherehekewa mwaka 1992, bado jamii ya Tanzania haijawa wazi kuhusu masuala haya. Katika mazingira ya kazi, hili halizingatiwi kwani ni taasisi chache ambazo zimeajiri mtaalamu wa kutoa msaada wa ushauri na wa kitabibu unaohusu afya ya akili kwa wafanyakazi.
Hofu ya COVID19 inawatafuna baadhi ya wafanyakazi ambao wanalazimika kwenda kazini kila siku kama vile hakuna tatizo lolote. Hofu hii ni kubwa zaidi kwa wale ambao wana watoto wadogo nyumbani na wanahudumia watu mbalimbali kila siku.
Lakini tatizo halipo kwa wale ambao wanaenda kazini tu. Hata wale ambao wanafanya kazi kutoka nyumbani wanapata shida kwani kutoka katika mazoea ya kila siku inaweza kuleta shida ya msongo wa mawazo, upweke n.k. Pia mazingira ya nyumbani yanaweza kuwa si rafiki na kupunguza ufanisi wa mfanyakazi hivyo kumpa hofu ya kupoteza kazi.
Vilevile wafanyakazi ambao wamepata COVID19 na kupona wanaweza kupata changamoto kurudi ofisini kwa kuogopa unyanyapaa ama kuwa na hisia kuwa ni kazi iliyopelekea wakapata maambukizi.
COVID19 pia imepelekea kupoteza kazi kwa baadhi ya wafanyakazi kutokana na sintofahamu iliyozikumba baadhi ya taasisi. Kuna taasisi ambazo zimewapa wafanyakazi taarifa za kusitisha utendaji baada ya miezi kadhaa hivyo wanafanya kazi huku wakijua watalazimika kusaka ajira mpya na kupelekea msongo wa mawazo.
Nini kifanyike?
1. Wahusika wajitahidi kufunguka na kuongea na watu wanaowaamini. Kuongea kunasaidia kupunguza mzigo wa mawazo.
2. Taasisi na Kampuni ziangalie namna ya kupata wataalamu wa afya ya akili kwa ajili ya kuwapa wafanyakazi msaada stahiki na hata kuwapa nyenzo za kuepuka matatizo ya akili katika kipindi hiki kigumu.
3. Taasisi zenye wafanyakazi wanaofanya kazi kutoka nyumbani zifanye mikutano ya mara kwa mara ya kujuliana hali na kujadili changamoto.

Upvote
0