Justine Marack
JF-Expert Member
- Jul 31, 2014
- 612
- 1,698
Hapa tuseme ukweli.
Tangu kuondoka Manara kuna mambo tayari Simba imerudi nyuma na kulingana na Yanga.
Kuna faida moja Manara ameiacha kwa Yanga nitaitaja baade.
Katika kipindi hiki cha usajili, tumezowea kuwa kipindi cha muhaho kwa pande zote mbili.
Manara akizowea kukoleza sana kwa kila nyanja ya burudani ya soka.
PAGE ZA MICHEZO
Kipindi cha Manara huu ndio wakati anagombana na waandishi wa habari wanao post usajili feki na tetesi kwa wachezaji wa Simba kwenda Yanga.
Tunakumbuka mwaka Jana aligombana sana kwa mchezaji wa Simba kupostiwaakiwa na wakiwa na jezi ya Yanga. Manara aliwaka moto sana na kugombana na akina Kitenge
Kuna wakati waandishi walifanya mambo kwa makusudi ili kumtafuta Manara awake, huku wao wakicheka na page zao kupata followers.
Kuondoka kwa Manara kutaathili hata baadhi ya page za michezo ambazo zilikua zinacharurana naye.
Watu walikua wakiona jambo fulani wanarudi kwenye page ya Manara kuangalia kuna anini ili wajue ukweli anajibu mapigo au la.
MAUZO YA JEZI
Mauzo ya jezi Mara nyingi huchangiwa na amsha amsha ya kuzodoana na kupondana kwa kila pande kutambia wengine.
Hapo hutokea kila timu kupata usajili wa kujivunia na hapo ndipo jina au Jezi ya Mchezaji huyo kutabiriwa kufanya vema kimauzo.
Mpaka sasa jina linalo Tarajiwa kuuza jezi zaidi ji DJUMA SHABAN wa Yanga. Hii imechangiwa na Manara kuiponda Yanga kuwa hawana uwezo wa kumnunua mchezaji huyo. Na tunaweza kusema hii pia ilichangia Yanga kuvunja benki na kukataa dharau za Manara mpaka wakamnunua. Na hii ndio tunaona namna manara ameacha ameifaidisha Yanga.
Tulitaraji kuona Manara akitafuta nani atakua Staa wa Upande wa Simba kuja kuleta Balance ya Djuma Shabani na hapo ndipo ungezijua Sifa za uongo na kweli za Peter Banda ambaye ni usajili mbadala wa Luis M.
Kuondoka Manara Usajili huu umepoa sana, yaani ulivuma siku ile ya kwanza tu na sasa Jamaa amepwaya kama hayupo.
Ni wakati huu ungeona Manara akiripoti Messi kutua Yanga tena akitumia misemo yake ya kuudhi na kukera. Hapa ndipo Yanga hujikuta wakienda Airport kumbeba mtu begani.
DESIGN YA JEZI MPYA
Muda sio mrefu jezi mpya zinatoka, na hapo ndipo huibuka ligi nyingine. Kuna jezi huwa inaonekana nzuri zaidi au kila timu kutafuta kasoro kwenye jezi ya mtani. Hapa ndipo jezi zenye Ramani ya Africa zinapigwa maneno mpaka zinakua mbaya.
Hapa ndipo jezi huitwa dera. Manara anaongoza hiyo ligi ya jezi.
Ile mineno ya Manara kuwa Jezi imejaa Mo, Mo, Mo kama za Sudan kiukweli Yanga hawakuwahi kuysema na hii ni sababu Manara alikejeli sana jezi ya Yanga na Ramani yao na na Yanga kutumia muda mwingi kujitetea na kusau kasoro ya jezi za Simba.
Ni Manara alileta mambo ya kuja na Diamond na Yanga kuja na Harmonize mpaka Harmo kuvunja kiuno.
BILIONI 20
Tayari tukio kubwa lilio subiriwa kwa miaka mingi limefanyika kinyoonge sana mpaka sasa tayari limesahaulika.
UTANI UMEPOA MITANDAONI
Moja ya kiashiria cha kupoa utani ni kupotea gafla kwa jina UTOPOLO.
Naona Kuna jina limeanzishwa kwa ajili ya kuwatania Yanga lakini limefeli mapema. "Mataputapu" nijina baya linakera lakini halifikii UTOPOLO. Yanga tayari wamepata afueni wnapumua kidogo. Natabiri IPO Sikh Nina utopolo litageuka kuwa la Simba, hii itakuja kama ikitokea Yanga wakifanya vizuri.
Sababu Yanga wanao watu wengi katika media kubwa. Lakini Manara aliwamudu. Sababu ya Manara kuwamudu ni kuwa anao Followers weni karibu Milioni tatu na nusu.
Sasa akiandika Utopolo wanasoma angalau watu milioni Tatu. Sasa leo unakuta kajitu kana followers mia mbili eti Kanaacha Utopolo kanaanzisha Utaputapu ha ha ha , nani ataijua hiyo taputapu?
Baada ya Manara Utopolo imepotea Mitandaoni
Ni takriban Siku kumi za Kuondoka Manara.
Kuna Mashabiki Maandazi wengi sana humu, wao wanatoa matusi bila kutafakari. Hao ndio walitukana sana badala ya kujibu kwa hoja.
Ni sababu Facebook imekua mtandao jalala unazoa vitoto vya mbwa na takataka nyingi
Mtu kama sio Shabiki Maandazi iwe Yanga au Simba lazima tukubali Manara ameacha pengo.
Acha Ushabiki maandazi na ujibu hoja za msingi au changia kwa hoja sio kubweka tu.
Je, nini tutegemee zaidi?
Credit Facebook
Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app