Athari za Mapungufu yaliyobainishwa katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa “force account”

Athari za Mapungufu yaliyobainishwa katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa “force account”

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mapungufu yaliyobainishwa katika utekelezaji wa miradi kwa utaratibu wa “force account”, yamepelekea kuwepo kwa athari zifuatazo:

a) Kuwepo kwa viashiria vya rushwa na udanganyifu katika mchakato wa ununuzi wa umma. Mfano; Kutilia shaka ushindani kwenye mchakato wa ununuzi katika miradi 21 yenye thamani ya TZS 2.13 bilioni inayotekelezwa kwa utaratibu wa “force account”, kutokana na nyaraka za zabuni zilizowasilishwa kuwa na miandiko inayofanana na kutokuwa na muhuri wa mtoa huduma

b) Kuwepo kwa upotevu/ubadhirifu wa fedha za umma. Mfano; Manunuzi yalifanyika kwa bei ya juu kuliko bei ya soko na kusababisha upotevu wa kiasi cha TZS 100.16 milioni ambazo zingeokolewa kama Sheria ya Ununuzi ya Umma 2016 kifungu 4A (3) (na marekebisho yake) ingezingatiwa.

c) Kukosekana kwa thamani ya fedha katika miradi iliyotekelezwa. Mfano; Majengo kupata nyufa muda mfupi baada ya kukamilika katika Shule za Sekondari Berege na Mazae zilizopo H/W Mpwapwa na Shule ya Sekondari Bulunde iliyopo H/Mji Nzega
 
Mkuu ni muda wa kugawana huu kila mtu ale kwa urefu wa kamba ake
Force Account ilitumika kipindi cha Magufuli chini ya Suleiman Jaffo ata hivo issue ya miandiko kufanana au ujanja ujanja katika issue za manunu ni maadili tu ndiyo kikwazo maana ata utumie mfumo gani ujanja ujanja utakuwepo tu.
 
Force Account ilitumika kipindi cha Magufuli chini ya Suleiman Jaffo ata hivo issue ya miandiko kufanana au ujanja ujanja katika issue za manunu ni maadili tu ndiyo kikwazo maana ata utumie mfumo gani ujanja ujanja utakuwepo tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndiyo hivyo mkuu we ingia kwenye hivyo vikamati vya ujenzi piga pesa kaa kimya usimwambie mtu.
 
Mbunge wa mpwawa, mkuu wa wilaya, madiwani ,mkurugenzi walikuwa wapi?

Mbona sehemu nyingine hayajatoa nyufa?

Bila force account serikali ingeweza kuhamia Dodoma??
 
Haya mambo ya manunuzi ya serikali ni changamoto.Kuna mzabuni tunampelekea quotation ajaze anAsema Mimi sifanyi hiyo kazi natafuta hela.
Yaani yeye ukienda kwake eti umpe tenda moja kwa moja
 
Serikali iliopita na hii tofauti ni magu tuuu.....kwa hizi ripoti wawajibike wote tuuu.... wasimsingizie marehemu (the law of collective responsibility should be adhered to).
 
Back
Top Bottom