Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Maziwa ya ng’ombe ni mojawapo ya chakula kilicho na virutubisho vingi vinavyofaa kwa afya ya binadamu.
Pamoja na ubora wake huu, aina hii ya maziwa huwa haifai kwa mtoto mwenye umri chini ya mwaka mmoja.
Huwa na kiasi kidogo cha madini ya chuma ambacho hakikidhi uhitaji wa mtoto, hali hii inaweza kumfanya apatwe na tatizo la kupungukiwa damu mara kwa mara.
Wastani wa asilimia 40 ya watoto chini ya mwaka mmoja wanaopatiwa maziwa ya ng’ombe hupatwa na tatizo la kuvujia kwa damu kwenye utumbo hivyo kuwafanya wapoteze damu nyingi kupitia choo. Aidha, huwa na kiasi kikubwa sana cha virutubisho vya Protini ambavyo humfanya mtoto apoteze kiasi kingi cha maji ili kuvitoa nje ya mwili. Hii inaweza kumfanya apatwe na upungufu mkubwa wa maji.
Maziwa haya ni mazuri kwa afya, hata hivyo yanapaswa kutolewa kwa mtoto baada ya kufikisha umri wa mwaka mmoja ili kumkinga dhidi ya athari hizi.
National Library of Medicine