chamilo nicolous
JF-Expert Member
- Mar 10, 2016
- 2,097
- 1,457
Serikali inapoendelea kukopa, jamii inaathirika vipi? Je, waziri wa fedha yuko sawa sawa kujitokeza adharani, na kukiri kuwa wataendelea kukopa na hakuna atakaeathirika?
Mchango wangu kuhusu hii mada ya mikopo ya Serikali katika sekta binafsi. Sekta inayo wahusu Watu binafsi na mashirika binafsi!
Kanuni za Kiuchumi zinatanabaisha Uchumi wa nchi siku zote serikali ndio mteja mkubwa. Ukisoma Dira na Mpango wa III wa maendeleo wa Taifa ukisoma na Sera zote za kisekta zinaitaja Sekta Binafsi kuwa mhimili wa Uchumi wa nchi.
Sekta ya Fedha kama jamii zingine za Biashara na Uwekezaji siku zote hupendelea kufanya Kazi na mteja wa uhakika mteja anayeaminika na huyu ni pamoja na Serikali.
Moja ya ATHARI ambazo ni za lazima pale Serikali inapojiendesha kwa mikopo au serikali anapokuwa mkopaji mkubwa Kwenye Sekta ya Fedha matokeo ni kwamba Benk nyingi zitapunguza mikopo Kwa Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Wawekezaji Binafsi Ili kuikopesha Serikali.
Matokeo yake Sekta Binafsi haitapata Fedha za kutosha kuendesha shughuli zake na hivyo:
1. Uwekezaji wa ndani utapungua.
2. Ubunifu utapungua na Sehemu kubwa ya Uchumi wa nchi utajielekeza kwenye trading tukitegemea sana bidhaa Kutoka nje ya nchi. Viwanda vya ndani vitashindwa kujiendesha. Ndo sababu kukopa kopa huku kwa Serikali ya Samia, husikii tena, nchi ya viwanda, oooh uchumi wa kati!
3. Tatizo la Ajira litaongezeka, viwanda vitakufa, umasikini utaongezeka na Pesa itakosa thamani.
Nashauri nafasi ya Gavana wa Fedha itazamwe upya na Wizara ya Fedha kama Wizara mama inayosimamia Uchumi wa nchi Nafasi ya Waziri itazamwe upya. Katika hili Waziri wa fedha umefeli.