Athari za msongo wa mawazo katika muonekano wako

Athari za msongo wa mawazo katika muonekano wako

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Ee unajua kuwa msongo wa mawazo unachangia mafuta yako kugoma na uso wako kujaa chunusi kwa wingi. Kila mmoja ana mtazamo wake kuhusu msongo wa mawazo ama kama inavyojulikana sana “ stress”. wengine wana stress za maisha, maradhi, ugonjwa, masomo na mambo kadha kadha. kwa kifupi kila mmoja na maana yake.

Hapa utajifunza ukiwa na stress ni nini kinatokea hadi unahisi kuchoka, huna hamu ya kula ama hamu ya kula inaongezeka zaidi, unahisi hasira wakati wote na mbaya zaidi unapata chunusi na yale mafuta yako mazuri unayopaka usoni siku zote yanagoma.

Kwenye mwili kuna vichocheo “homoni” tofauti tofauti ikiwemo homoni ya msongo wa mawazo iitwayo Cortisol humwagwa katika damu pale tu unapoingia kwenye mstuko wa kimawazo.

Athari za homoni hii mwilini Hutegemea sana Muda ambayo homoni hii inadumu kwenye damu na Kiwango cha kuisisimua (Mara kwa mara). Kwa hio kama una ingiza mwili wako kwenye msongo muda mwingi ndivyo unavyopata athari za Homoni hii.

Homoni ya msongo inapomwagwa kwenye damu hukaa kwenye damu kwa dakika hadi 100 karibia masaa mawili ndipo inamaliza nguvu na kuondolewa. Ina maana muda wote huo inaleta madhara mwilini.

Mawazo Yanaweza Kukufanya Muda Wote Homoni hii ikiendelea Kuleta madhara. Na kumbuka Ikisha temwa haiondoki au kushuka hapo hapo. Inadumu muda wote huo ikileta athari mwilini. Kiafya haitakiwi uwe unaisisimua mara kwa mara hadi sababu maalumu mfano Umekutana na nyoka au unataka kumkimbia adui anayetaka kukukata panga nk.

Msongo wa Mawazo kwa sababu unasabisha mvurugiko wa homoni ndio unasababisha Chunusi ndogo, na wengine hutoka chunusi kubwa zaidi, na kwa sababu hiyo hiyo ndio hata ukipaka mafuta yanakukataa, yaani hayaendi kufanya kazi yake kama mwanzo maana wewe umeshaharibu mfumo mzima wa upokeaji wa kipodozi husika kwa kuwa mawazo uliyonayo yanapandisha homoni ya mawazo yenye kuleta mvurugiko wa homoni na madhara mengine ni kama ifuatavyo

1. Unaongeza Uzito kwa kasi

2. Msongo wa mawazo unashusha nguvu za kiume

3. Msongo wa mawazo unapandisha sukari na presha

4. Msongo wa mawazo unavuruga homoni za kike

5. Msongo wa mawazo unapanua moyo na kuleta shambulio la moyo

6. Msongo wa mawazo unaweza kukufanya ufikirie kujiua

7. Msongo wa mawazo Unakukosesha marafiki hata wazuri.

8. Msongo wa mawazo unafanya hata nywele zako ziwe zinakatika katika kwa sababu ya mvurugiko wa homoni.

Suluhisho:

Jitahidi kwa namna yoyote unayoweza kujilinda na msongo wa mawazo “ stess” utakuwa salama kwa afya yako na ngozi yako kwa ujumla!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu msongo umesahau

Msongo huketa mvi mapema

Msongo huleta bleed nyingi tena kwa mvurugiko

Msongo hupoteza usikivu

Msongo hukondesha uso tu😜

n.k
 
Ni kweli kabisa kaka umenena vema;

Mtu akiwa na msongo wa mawazo inapelekea mwili kuacha kufanya shughuli za starehe/luxury na kuamua kutilia mkazo/focus kwenye kujiokoa[survival]. Inaleta hasara sana kwenye urembo na umbo. Chanzo kikuu cha stress ni ufahamu wa taarifa nyingi mbovu na za hatari na za kutisha. Hizi zikiwa nyingi kuliko zile njema, mwili unaegemea kwenye stress zaidi badala ya afya na utulivu.

Nimejaribu kutoa baadhi ya mbinu za kujiweka katika hali nzuri hapa[stories of change] Mbinu ya kutumia akili na utashi binafsi kuiendesha afya na mwili wako - A biological appeal to free-will
 
Unaongeza Uzito kwa kasi
Ebhana asante sana, maana kuna wakati ukiwaambia watu kwamba stress nyingi zinaongeza unene watu wanakuangaliaaa halafu wanasema 'uchizi unakunyemelea'. Ooh mtu ananenepa sababu hana stress!!

Au mwingine anampa ushauri mwenzake eti 'ukitaka kitambi kiishe kopa mkopo benki halafu kauhonge, stress zitakukondesha!' Hizi ni imani potofu zinazotumia mifano ya kale katika mazingira ya kisasa.

Ni kweli kukonda na kunenepa yote yanaweza kuwa matokeo ya stress. Kwa mazingira yetu ya kisasa hiyo ya pili ndiyo inahusika zaidi. Inategemea tu na mwitikio wako upoje.
 
Ukweli mtupu, mpaka wajiuliza haya mafuta haya mbona yamenigomea this time [emoji23]
 
Hebu ngoja nijipapase Usoni.

Afadhali, sina hata Chunusi moja
 
Na wale wanaosema Chunusi za Balehe nayo hii imekaaje?
 
Ebhana asante sana, maana kuna wakati ukiwaambia watu kwamba stress nyingi zinaongeza unene watu wanakuangaliaaa halafu wanasema 'uchizi unakunyemelea'. Ooh mtu ananenepa sababu hana stress!!

Au mwingine anampa ushauri mwenzake eti 'ukitaka kitambi kiishe kopa mkopo benki halafu kauhonge, stress zitakukondesha!' Hizi ni imani potofu zinazotumia mifano ya kale katika mazingira ya kisasa.

Ni kweli kukonda na kunenepa yote yanaweza kuwa matokeo ya stress. Kwa mazingira yetu ya kisasa hiyo ya pili ndiyo inahusika zaidi. Inategemea tu na mwitikio wako upoje.
Kweli kabisa
Stress zinaweza kusababisha chakula kiwe faraja yako hata hasira pia.
Mi nikiwa na stress nataka kula kula.
 
Kweli kabisa
Stress zinaweza kusababisha chakula kiwe faraja yako hata hasira pia.
Mi nikiwa na stress nataka kula kula.
Exactly..... ndivyo ilivyo kwa walio wengi tu. Sema wengine ile kutambua ni kwa nini wanafanya nini wanakuwaga hawawezi.

Hongera kwa kujua, hapo unao uwezo wa kujiendesha maana unajijua kiasi kikubwa👊
 
Kwa hiyi stress inakondesha au inanemeesha ipi ni sahihi
 
Kweli kabisa
Stress zinaweza kusababisha chakula kiwe faraja yako hata hasira pia.
Mi nikiwa na stress nataka kula kula.
Mi nikiwa na stress napiga sana nyeto mpaka inafika kipindi hazitokii [emoji58]
 
Back
Top Bottom