Athari za mtoto kuchelewa kulala usiku

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


T
aarifa iliyotolewa na shirika la habari la Uingereza BBC, Julai 8 kuhusu utafiti uliofanyika nchini Uingereza uliowahusisha watoto 11,000 wakifuatiliwa kuhusu ratiba zao za kulala na kupima uwezo wa bongo zao.
Watafiti

hao walisema ya kwamba wale watoto waliolala baada ya saa tatu usiku na waliokuwa hawana ratiba maalumu walikuwa na alama za chini kwenye hisabati na uwezo wa kusoma.
Na vilevile waliripoti kuwa ni vigumu ubongo

kujifunza vitu vipya kutokana na ukosefu wa usingizi. Walichukua watoto wa kati ya miaka 3, 5 na 7 wakifuatilia uwezo wao wa kujifunza ukilinganisha na ratiba zao za kulala. Ratiba ilikuwa mbaya zaidi kwa watoto wa miaka

3. Na mpaka wanapofika miaka saba huwa na ratiba inayoeleweka kati ya saa moja na nusu usiku na saa mbili na nusu usiku.


Waliokuwa na ratiba nzuri ya kueleweka walifanya vizuri zaidi katika hisabati na kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma ukilinganisha na wenzao wasio na ratiba ya kueleweka na waliokuwa wanachelewa kulala .
Kuhusu

kupungua uwezo wa ubongo athari zilionekana zaidi kwa wasichana ukilinganisha na wavulana. Utafiti huu uliofanywa na Prof. Amanda Sacker wa chuo kikuu cha London alisema kuwa vilevile mazingira mabaya ya

familia zetu huweza kupelekea hali hii na aliijumuisha katika sababu za kupunguza uwezo wa ubongo.
Kitu Muhimu cha kuzingatia ni watoto kulala mapema na kumbuka bado hujachelewa, ni vizuri kumuwekea ratiba

nzuri ya kulala mtoto, na hakukuwa na usha
hidi wa matokeo kuwa mazuri mtoto akilala kabla ya saa moja na nusu.
Kwa ujumla ili mtoto afanye vizuri darasani ni vema apate usingizi mnono usiku.Source: BBC News - Late nights 'sap children's brain power'

 
Naweza kukubaliana nao, kwa sababu mimi mwenyewe nimejitahidi kuzingatia ratiba ya kulala tangu akiwa mdogo. Hivyo nimeona hata maendeleo yake darasani anajitahidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…