Athari za muda mfupi na mrefu za uchizi wa kiroho, Tanzania

Athari za muda mfupi na mrefu za uchizi wa kiroho, Tanzania

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Kidunia, kutokana na maendeleo, sayansi na teknolojia, ongezeko la ukwasi wa vitu yamewafanya watu kuwa na maswali mengi kuliko majibu kumekuwa na mahitaji makubwa sana ya kuelewa zaidi ya kile kilichozoeleka kueleweka. Kumekuwa na mashaka makubwa sana juu ya aina ya uelewa uliopo juu ya kila kitu jambo lililosababisha watu kutamani kelewa nguvu zinazosukima matokeo hususani katika ulimwengu wa roho.

Miaka kadhaa iliyopita Afrika kulizuka wimbi kubwa la mahitaji ya masuala ya kiroho na jicho la tatu. Kupitia kumbo hilo la wakati waliibuka watu wengi waliojinasibu na utoaji wa elimu ya masuala ya kiroho. Wapo waliojikita katika matumizi ya njia ya tahajudi na wengine kutumia jina la "meditation" lakini wapo waliojificha kwenye dini hususani imani za kilokole na kujiita manabii.

Nchini Tanzania ombwe hili la mahitaji ya kutaka kujua masuala ya kiroho hususani Kwa vijana Tanzania limekuwa likikua kila uchao jambo lililosababisha kuzuka kwa kundi kubwa la watu waliochukulia mahitaji hayo kama fursa kwao.

Kiwango cha matamanio na mahitaji ya vijana wengi nchini juu ya mafanikio hususani ya vitu "material wealth" kimefikia hatua ambayo ni ya uchizi wa kiroho kwa sababu ya kufifia kwa tabia ya kuhoji na kujihoji iliyojengwa na watu waliojibatiza kuwa ni watumishi wa Mungu.

Waumini wengi hususani ni kama wamesafushwa akili, wapo tayari kufanya chochote kile wanachoambiwa na mtu waliyeamua kumuamini kama nabii wao. Huu ni uchizi wa kiroho na ndiyo hatua ambayo vijana wengi wamefikia.

Kuna hatari kubwa kama hali hii ikiachiliwa kuwa ilivyo Kwa sababu watu wanaposafishwa akili wanaweza kufanya chochote kile watakachoekekezwa na aliyewasafisha bila kuhoji wala kupima. Ikiwa mtu anaweza kusafishwa akili na kushauriwa aichome moto zawadi aliyopewa kwa sababu kiroho inamzuia kufanikiwa ni dhahiri mtu huyo au wa aina hiyo anaweza kutekeleza jambo jongine la hatari zaidi atakaloelekezwa.

Vikosi vinavyotekeleza maovu mengi katika nchi nyingi duniani ukifuatilia utagundua watu wake husafishwa kwanza akili na kukaa katika utekelezaji wa maelekezo yoyote watakayopewa. Tabia hii ya kupumbaza waumini na washirika chin ya kivuli cha masuala ya kiroho inaweza kuandaa vijana amba wanaweza kuja kufanya mambo ambayo yataharibu zaidi.

Tunashuhudia sasa manabii wenyewe Kwa wenyewe wakijigunua uchafu wao na namna wanavyowaghilibu akili waumini wao na kuwafanya kama kondoo wao wa kafara. Huu ni wakati muhimu sana wa kujitathmini kama Taifa tunakoelekea.
 
Sasa kama wachungaji wao hawawahubirii injili ya kweli wataweza kupambanuaje mafundisho ya kweli na ya uongo? Wataishia tu kuwa mateka wa imani potofu
 
Kama kipindi cha yule jamaa wa Uganda akawaambia mwisho WA Dunia umefika tujichome moto sijui tuwai wapi matokeo ndo hayo wanafanya kila wanachoambiwa
 
Tunaweza tukachukulia masihara mtu kuchoma gari porini, ikumbukwe mtu huyo anaweza kuichoma hata familia yake akielekezwa na aliyemsafisha akili...."........an opium of mind"..
 
Kama kipindi cha yule jamaa wa Uganda akawaambia mwisho WA Dunia umefika tujichome moto sijui tuwai wapi matokeo ndo hayo wanafanya kila wanachoambiwa
Naam,
Tusipuuzie hii hali hata kidogo
 
Kuna kisa kimoja kilitokea huko mme na mke watoto, walikuwa wanasali kwa mchungaji mmoja mwanamke yule mama alikuwa anakuja mpaka kwao Nyumbani akawa yupo beneti sana na baba wa Familia mwisho sijui alikuwa anamsomea vifungu Gani vya biblia yule mama, mme akaua watoto tofauti na mke pia, na yeye akajitoa uhai hiki kisa nilisoma nadhani kilitokea kenya
 
Back
Top Bottom