Athari za uchakataji upya wa matokeo kidato cha iv 2012

damashizo

Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
61
Reaction score
15
Nimetafakari na kuchunguza na mwisho nimebaini zifuatazo ni athari za uchakataji upya wa matokeo ya kidato cha IV 2012.

Mosi Baraza la mitihani litatakiwa lirudishe gharama zote zilizotumika na baadhi wa wahitimu waliodhaniwa kuwa wamefeli na wakaamua kutumia fedha kwaajili ya kujisajili kama watahiniwa wa kujitegemea ili kufanya mtihani tena 2013 hususani ikibainika kuwa wamefaulu.

Pili taasisi mbalimali za kielimu walishatoa matangazo ya nafasi mbalimbali za masomo mfano vyuo vya ualimu, vyuo vya afya, kilimo n.k. Hii inamaanisha kwamba muda wa kuwasilisha maombi itabidi uongezwe hivyo zoezi la kuwachagua litachelewa na mwisho wanafunzi watachelewa kuanza masomo na mwisho mafunzo hayatakamilika.


Pamoja na pointi hizi wanajf waweza ongeza athali zingine ili kuisaidia serikali yetu itambue na mwisho wafanyie kazi.
 
Waziri wa elimu,naibu wake na katibu mtendaji wa baraza la mitihani watatakiwa kushitakiwa kwa kusababisha vifo vya wale walio jiuu kutokana na matokeo mabovu
 
Hapa wanataka kuziba nyufa iliyojitokeza tu hii ni baada ya watu kulalamika sana, haingii akilini kabisa swala la kurekebisha matokeo ni mawazo ya ajabu sana kuwahi kutokea katika karne hii.
 
hiyo wazungu wanaita "revolution" hasa ktk mwaka 2012 sabab migomo mingi mwaka huu madaktari,walimu pia zoez la sensa swali la kujiuliza kwa wale wanafunz wa shule za kata ilikuwaje katika kusoma kwao?na kama tunavyofamu ufundishaji wa shule hiz je wanfunz walimaliza topic walizotakiwa kusoma?yaaaaaan! daaaah! ni noooumaa!
 
Kama wanavyodai kuwa Lukandala na Ndalichako walitumia alama za marks mpya badala za zamani ambazo zilichangia kufeli kwao.
 
Siasa imeingizwa, tunasubiri matokeo ya 2015 watakapo kuwa wanamaliza F6 mambo yatajirudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…