Athari za uchumi imebadilisha malezi na maadili kwa watoto

Athari za uchumi imebadilisha malezi na maadili kwa watoto

Shining Light

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2024
Posts
406
Reaction score
523
Hali ya uchumi imekuwa ngumu, na zamani, wanamama waliweza kukaa nyumbani na kulea watoto wao vizuri kwa kujishungulisha kwa biashara ndogondogo ana kuweza pia ungalia na kuwa na muda mrefu na watoto wao. Hata hivyo, sasa inawalazimu kuwa na watu wa kuwasaidia kulea watoto kama dada wa kazi au wengine hulelewa na mabibi zao.

Kwa hali hio imewalizimu wanamama kupaswa pia kufanya kazi. Kwa sababu hii, watoto wengi wamekosa ukaribu na wazazi wao, na wazazi pia wameshtushwa na mambo watoto wao wanafanya hasa wakitwa mashuleni kuwa watoto wao wamefanya makosa ya aina fulani hii inasababishwa kwa kuwa hawana uhusiano wa karibu na watoto wao.

Pamoja na hayo, changamoto nyingine inayoibuka ni kwamba watoto wanakosa maadili na mwongozo muhimu ambao ungetolewa na wazazi wao kuendana na mila na desturi ya jamii iliyo tuzunguka. Malezi ya watoto sasa yamekuwa yakitegemea zaidi walimu, walezi, na vyombo vya habari, ambavyo wakati mwingine havina maadili sawa na yale ya nyumbani.

Teknolojia na mitandao ya kijamii pia zimechukua nafasi kubwa katika maisha ya watoto, na kuwafanya kuwa na maadili na mienendo tofauti na matarajio ya wazazi wao. mambo ya utanda wazi yamekuwa yakisababisha mmonyoko wa madili mengi na mienendo ya jamii kuwa tofauti sana.

Pia, tegemeo la kulisha familia, kuhudumia familia kwenye mavazi, malezi, starehe, elimu imesababisha uwajikibaki wa wazazi wawili kufanya kazi umeongeza msongo wa mawazo, na kupunguza muda wa familia kuwa pamoja.

Hii imeathiri vibaya uhusiano wa kifamilia na malezi ya watoto, huku baadhi ya watoto wakihisi kutengwa na wazazi wao. Kwa hali hii, familia nyingi zimekosa utulivu na mshikamano uliokuwepo zamani, na kuleta changamoto kubwa katika kufanikisha malezi bora ya watoto, hata hivyo pia unasababisha watoto kutumia vilevi umri mdogo na pia kusabisha sonono ambayo inaathiri maendeleo yao ya shule.
 
Nimethibitisha hili kwangu na mwaka huu umekuwa wa kupambana kuweka mambo sawa hadi hii october to november ndiyo nimeona mwanga kiasi na penyewe kwa mbinde. Kama wazazi mpo mbali na watoto tambueni kwamba wataharibika tu unless uwe umewaweka mahali bora kimalezi ila kama wapo nyumbani tena wenyewe umekwisha. Watakuwa majambazi , walevi, wavuta bangi na hata uzinzi wangali wadogo kabisa hadi ushangae
 
Back
Top Bottom