SoC02 Athari za uraibu kiafya na kiuchumi kwa ujumla

Stories of Change - 2022 Competition

Cwt_chess

Member
Joined
Jul 24, 2022
Posts
5
Reaction score
10
Uraibu hutazamwa kama ugonjwa au utumwa wa ndani unaotokana na hali ya kuzoea kufanya kufanya kitu chenye madhara bila kujizuia . mara nyingi watu huzingatia Zaidi uraibu wa dawa za kulevya na kuchukulia ulevi kama tabia lakini kisichojulikana ni kua kuna uraibu wa mambo mengi kama vile uraibu wa madawa ya kuevya , kamali, pombe, matumizi ya mitadao ya kijamii hasa kwa kuchati,uraibu wa kutizama video za ngono,uraibu wa kutizama sinema na uraibu wa kula pamoja na kununua vitu visivyo na ulazima.
Uraibu wa matumizi ya dawa za kulevya ;

Uraibu wa dawa za kulevya
Huathiri vijana kwa kasi kubwa , matumizi ya cocaine, bangi, mirungi n.k bila kibali cha daktari hupelekea watu hususani vijana kujipa vipimo na dawa zisizo hitajika na miili yao , madawa hayo huathiri ubongo na utendaji kazi wake , madawa mengine hupumbaza , mengine hupunguza maumivu , kubadili hisia , kupoteza kumbukumbu. Matumizi ya dawa hizi hupelekea vijana kujihusisha na wizi au njia mbalimbali ili kuweza kujipatia dawa hizo. Wengi waingiapo katika uraibu hushindwa kufikiri sawasawa na kila mara huhisi kushindwa kustahimili bila dawa hizo hivyo hufanya kila namna ili waweze kujipatia dawa hizo nyingi huuzwa kwa njia za panya kwakuwa si halali. Vijana wanategemewa kuwa taifa la kesho lakini kundi kubwa hupotea napojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya.

Uraibu Wa Pombe
Uraibu wa pombe hutokana na matumizi ya pombe kupita kiasi , hii hutofautiana na tabia ya mtu kunywa pombe kama kiburudisho . Uraibu huu humfanya mtu awaze pombe na kutamani kuipata kila wakati , uraibu huu waweza kuathiri vijana na hata watu wazima. Matumizi ya pombe kupita kiasi hathiri afya na utendaji kazi kwa ujumla . Kwa wafanyakazi binafsi au wa serikali utendaji wao wa kazi hupungua kwakua pombe au kilevi chochote humfanya mtu kutofikiria vizuri hivyo kupuuza majukumu yake ya kila siku na kujikita Zaidi na pombe.

Uraibu wa matumizi ya mitandao ya kijamii, sinema na ngono
Mambo haya yanamuingiliano , japo sio sana lakini asilimia kubwa ya watu hutumia mitandao ya kijamii kwaajili ya biashara na kujitaftia fursa. Kundi linalobaki hutumia mitandao hiyo kutizama video za ngono, sinema kuchati bila kikomo(kila wakati kutumiana jumbe mbalimbali zisizo na faida) na wengine hutumia mitandao ya kijamii kutumiana video hizo. Uraibu wa ngono haumaanishi mtu kufanya ngono tu, hata kuangalia video hizo bila kujizui ni uraibu wa ngono pia .

Vitendo hivyo huathiri afya ya mtu kisaikolojia na utendaji kazi wao , watu haw ahata wakiwapo makazini hupumzisha kazi na kuanza kutumia mitandao ya jamii na wengine hujikita katika kuangalia video hizo zenye dhima za kingono. Wengi hushinda siku nzima wakiangalia sinema bila kujihusisha na kazi yeyote , jopo la vijana wengi hujihusisha na uagaliaji wa sinema usio na tija bila kujishughulisha na shughuli zozote za kuwaongezea kipato wala kukuza uchumi wao wenyewe.

Uraibu wa kamali
Uraibu hawapata watu wa aina zote , matajiri kwa masikini pia , kamali huchezwa na watu mbalimbali vijana kwa wazee . Kamali ni aina ya mchezo ambao huchezwa kwa njia ya hela. Watu wapatapo uraibu wa kamali , huiba, hukopa bila kulipa na wengine huuza vitu vyao vya thamani ili kuendelea kucheza mchezo huu wakitegemea kupata fedha Zaidi ya walizo toa. Huwa hawajali kiasi cha pesa walichopoteza badala yake huwaza namna ya kupata fedha Zaidi kwa kuendelea kucheza mchezo huo. Na mwisho hushusha uchumi kwa madeni , wengine hufukuzwa kazi kutokana na wizi na wengine huishia lumande. Haya yote husababisha uyumbaji kiuchumi kwa kuwa nguvu kazi huporomosha uchumi badala ya kuukuza.

Uraibu wa kula na kununua vitu visivyo na umuhimu
Uraibu wa kula huhusisha ulaji uliopitiliza , kutofautiana na ulafi, uraibu wa kula humfanya mtu kula vyakula hivyo mara kwa mara bila kukiacha bila kujali madhara ya vyakula hivyo mfano; unywaji wa soda kila mara au kula vyakulavisivyo na manufaa hasa vyenye sukari mara kwa mara bila kuweza kuacha. Ununaji wa vitu visivyo vya muhimu waweza kuwa uraibu pia hii hupelekea watu kutumia pesa nyingi kununua vitu wasivyo hitaji na hivyo kupelekea mtu kushuka kiuchumi.

JE, NAWEZAJE KUEPUKA AU KUACHANA NA URAIBU?

Uraibu haathiri afya ya saikolojia Zaidi , na hivyo matibabu yake huwa ya kisaikolojia Zaidi. Ni vigumu mtu kutambua athari ya kitu anachokipenda na hata wanaotambua huwa ni vigumu kuacha kutokana na uhitaji wa kitu hicho . Nchi yetu ni moja ya nchi zenye nyumba za kurudisha fahamu yaani kwa kitaalamu soba house( sober house) hii ni sehemu yenye wataalamu waliobobea kurudisha watu katika fahamu zao na kuushinda uraibu waliokuwa nao. Maranyingi wataalamu hawa hujumuisha watu waliopitia hali fananishi kama mifano ya kuwasaidia watu kupambana uraibu huo. Ni jukumu la mtu mwenye uhitaji wa matibabu au familia ya muathirika wa uraibu kutembelea kituo cha afya cha karibu ili kuelekezwa namna ya kupata msaada katibu nyumba za kurudisha ufahamu wa mhusika.

Nafasi ya Serikali na wananchi katika kupambana na uraibu
1. Serikali inategemewa kupambana kwa kina katika uingizaji na matumizi ya madawa ya kulevya kwakuwa hii ndio sababu au uraibu ulioshika kasi nchini. Wananchi wakishirikiana na polisi kukamata wauzaji na watumiaji wa madawa ya kulevya kutapunguza athiriko la watu wengi kwa madawa hayo. Pia kupeleka watumiaji hao katika nyumba za kurudisha ufahamu badala ya kuwafunga gerezani ambako hawapati msaada wowote wakiafya.

2. Wananchi kusaidiana wao wenyewe na ndani ya familia zao pia kushinda uraibu mbalimbali na pia kuwapendeka ndugu, jamaa au hata majirani waliokwisha athirika na uraibu wowote katika nyumba za kurudisha ufahamu
 
Upvote 8

Vote poll ipo in active
 
Vote yako kesho nikiwa kwenye PC
 
Back
Top Bottom