SoC04 Athari zilizotokana na mvua, nini kifanyike kuhakikisha madhara hayo hayatokei tena ili kusaidia kuijenga tanzania tuitakayo

SoC04 Athari zilizotokana na mvua, nini kifanyike kuhakikisha madhara hayo hayatokei tena ili kusaidia kuijenga tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 7, 2024
Posts
6
Reaction score
2
UTANGULIZI
Mnamo mwezi agosti mwaka 2023 mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) ilitoa tahadhari kuhusu mvua za El nino zitakazo anza kipindi cha vuli kuanzia wiki ya pili ya mwezi october mpaka wiki za mwanzo ya mwezi January 2024 na miezi mingine ya mwaka huo. Mamlaka hiyo ilitoa tahadhari kuwa mvua hizo za El nino zitasababisha maafa makubwa maadhi ya maeneno nchini, ikiwa eneo walilolitaja kuwa kwenye hatari hiyo ni pamoja na mkoa wa Kilimanjaro, Pwani na maeneo ya kusini.
Screenshot_20240427-120954_1.jpg

Chanzo (TMA).

Tumeshuhudia maafa hayo yakitokea baadhi ya mikoa nchini Tanzania, ikiwa ni baada ya mvua kubwa ambazo zinaendelea kunyesha nchini Mikoa iliyoathiwa sana na mvua ni pamoja na Morogoro, Arusha, Mbeya, Manyara, Dar es salaam, Pwani, Lindi, Kagera, Kilimanjaro, Geita, Songwe, Rukwa, Kigoma, na Shinyanga. Maeneo ambayo yamethirika katika mikoa hiyo ni pamoja na vifo vya binadamu na wanyama, uharibifu mkubwa wa miundombinu hususani barabara, madaraja na miundombinu ya umeme, upotevu wa mali zikiwemo nyumba kubomoka,magari,vyombo vya majumbani,hifadhi ya chakula,mashamba kuharibiwa, kupunguza uzalishaji kwenye baadhi ya viwanda nchini.

img_1714210209314.jpg

Chanzo,(magazeti ya habari Leo,nipashe na Majira.)

Katika kipindi cha miaka mitano nchini Tanzania, tumeshuhudia maafa yatokanayo na mvua yakiripotiwa. Baadhi ya maeneo maafa hayo yamekua yakijirudia rudia, na baadhi ya maeneo mapya yakiibuka
img_1715104572302.jpg

Chanzo.( Mwanamchi, trt Africa).
Kwa mujibu wa azam tv, wanaonyesha takiwamu za maafa ya mvua za el nino mpaka sasa zikiwa ni, zaidi wa watu 155 wamepoteza maisha, zaidi ya kaya 51000 zimeathiriwa, zaidi ya watu 200000 wameathirika na mvua,zaidi ya watu 236 wamejeruhiwa, na zaidi ya nyumba 10000 zimeharibika kutakana na mvua zinazoendelea.

NINI KIFANYIKE NA KUTEKELEZWA ILI MAAFA YATOKANAYO NA MVUA YASIJIRUDIE MARA KWA MARA NA KUHARIBU RASILIMALI ZENYE TIJA KWENYE NCHI.
A. Serikali iunde Wizara inayojitegemea itakayo shughulikia masuala ya hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na maafa,itakayoitwa Wizara ya hali ya hewa, mabadiliko ya tabia nchi na maafa. Mbali na kuwa serikali imeunda taasisi ambazo zinashughulikia masuala ya hali hewa na mabadiliko ya tabia nchi ambazo taasisi hizo ni pamoja na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), ambayo inasimamia huduma na utabiri wa hali ya hewa kikanda, katika usafiri wa anga, tahadhari za tsunami, hali ya hewa ya maji, hali ya hewa ya kilimo na huduma za klimatolojia. Pia tume mbali mbali na Wizara kadha wa kadha zimekua zikifanya kazi pamoja na taasisi hizo katika kutatua changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi. Ofisi ya Waziri Mkuu pia imekua ikijihusisha kwenye utatuzi na kukabili madhara hayo. Licha ya Wizara hizo kushughulikia masuala ya hali ya hewa ambayo yamekua yakileta madhara miaka na miaka bado imeshindwa kufanya na kusimamia kikamilifu sehemu hii ambayo ni hatari Kwa maendeleo ya Nchi.Hivyo ushauri wangu ni kwamba serikali iunde Wizara inayojitegemea itakayosimia, yenyewe, mausala yote yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na athari zake, kufanya hivyo tutasaidia katika kujenga Tanzania tuitakayo Kwa sababu zifuatazo.
1) Wizara itatengewa bajeti, hivyo bajeti hiyo itatumika bila mgawanyo moja kwa moja kwenye kushughulikia masuala yote yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na kutatua athari mbali mbali, na kuitua mzigo Wizara mbalimbali zinashughulikia mambo haya.
2) kuongezea Kwa ufanisi katika huduma za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na utoaji rasmi wa taarifa muhimu za hali ya hewa na kuwafikia walengwa.

3) Kuongezeka kwa wataalamu wa hali hewa nchi nzima, ambao watakua wakitoa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na namna mbali mbali za kujikinga na athari hizo.

B)Kutokana na kuwa hali ya hewa kutotabirika kwa sababu ya kubadilika badilika kwa misimu ya hali wa hewa kwa miaka husika, Kwa maana ya kadiri miaka inavyozidi kwenda ndivyo hali inavyozidi ama kuwa nzuri zaidi au mbaya zaidi. Hivyo serikali ikishiriana na mamlaka husika inatakiwa kuhakikisha nchini TANZANIA wananchi wake wapate elimu ya awali ya kujikinga na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa, ambayo elimu hiyo iwe maalum na kuwekwa kwenye mitaala ya elimu kuanzia msingi na sekondari ambayo itaitwa( Mabadiliko ya tabia nchi, madhara yake na namna ya kujikinga)Ili kuwajengea uwezo watanzania katika kujikinga na madhara yatokanayo na mvua na maafa mengine ikiwemo ukame.Elimu hiyo itasaidia kupunguza maafa hasa vifo na upotevu wa mali unaopelekea kudidimiza nchi badala ya kuneemesha na hapo tutatengeneza Tanzania nzuri tuitakayo.

C. Kupima na kugawa maeneo mapya kwa wananchi ambao wako katika maeneo yenye hatari ya kupata athari hizi, kuchukua hatua za haraka kuwatoa katika maeneo hayo itasaidia kupunguza gharama ambazo zitatumika baada ya maafa. Wizara ya Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi ikishiriana na TMA ifanye tathmini ya maeneo yasiyo na hatari ya mafuriko na kuchukua hatua za kugawa kwa wananchi maeneo hayo. Kama imewezekana Kwa msomera na hili litawezekana.

Hitimisho.
Hatuwezi kuwa na Tanzania tuitakayo yenye matunda kama kila mwaka serikali itakua inashughulika na madhara yatokanayo na mvua ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kuepukika kabla ya kutokea. Hivyo serikali ichukue hatua hizi za haraka Ili kunusuru mali, amali na rasilimali za taifa hili kwa maendeleo ya wote.
 

Attachments

  • img_1715104572302.jpg
    img_1715104572302.jpg
    717.7 KB · Views: 4
Upvote 1
Kuongezeka kwa wataalamu wa hali hewa nchi nzima, ambao watakua wakitoa elimu ya mabadiliko ya tabia nchi pamoja na namna mbali mbali za kujikinga na athari hizo
Hao wataalamu tuwajaze kwenye tafiti na uvumbuzi wa masuluhisho ya maafa, mfano miundombinu zaidi.

Maana kwa kusema kutoa elimu hivi kwani TMA imekuwa na upungufu huo ama.....? maana ikishawekwa taarifa katika TV au redioni ni tayari wameshawafikia watu wote. Na watu nao watake kujifunza maana.

Tukirudi kwenye elimu, sawa basi wataalamu wajikite pia katika content creation. Ili habari ziwe kamilifu badala ya kutishiatishiana hali inayoibua dhihaka.

Hivyo serikali ikishiriana na mamlaka husika inatakiwa kuhakikisha nchini TANZANIA wananchi wake wapate elimu ya awali ya kujikinga na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi na hali ya hewa, ambayo elimu hiyo iwe maalum na kuwekwa kwenye mitaala ya elimu kuanzia msingi na sekondari ambayo itaitwa( Mabadiliko ya tabia nchi, madhara yake na namna ya kujikinga)Ili kuwajengea uwezo watanzania katika kujikinga na madhara yatokanayo na mvua na maafa mengine ikiwemo ukame.Elimu hiyo itasaidia kupunguza maafa hasa vifo na upotevu wa mali unaopelekea kudidimiza nchi badala ya kuneemesha na hapo tutatengene
Naona umelizungumzia hapa, vizuri, elimu kamilifu ya wakati wote iwapatie wananchi wote. Vitu kama skauti, jeshi la kujenga taifa pia vina nafasi yake katika hili.

Hatuwezi kuwa na Tanzania tuitakayo yenye matunda kama kila mwaka serikali itakua inashughulika na madhara yatokanayo na mvua ambayo kwa kiasi kikubwa yanaweza kuepukika kabla ya kutokea. Hivyo serikali ichukue hatua hizi za haraka Ili kunusuru mali, amali na rasilimali za taifa hili kwa maendeleo ya wote.
Yas, mifumo iwekwe sawa kukabiliana na chochote wakati wowote. Tujiulize na tuiulize serikali: au hili la watu kutojiandaa vema ni 'dili' ili kupata nafasi ya kuchota pointi muhimu kwa kuonesha matendo ya huruma kwa wahanga?
 
Hao wataalamu tuwajaze kwenye tafiti na uvumbuzi wa masuluhisho ya maafa, mfano miundombinu zaidi.

Maana kwa kusema kutoa elimu hivi kwani TMA imekuwa na upungufu huo ama.....? maana ikishawekwa taarifa katika TV au redioni ni tayari wameshawafikia watu wote. Na watu nao watake kujifunza maana.

Tukirudi kwenye elimu, sawa basi wataalamu wajikite pia katika content creation. Ili habari ziwe kamilifu badala ya kutishiatishiana hali inayoibua dhihaka.


Naona umelizungumzia hapa, vizuri, elimu kamilifu ya wakati wote iwapatie wananchi wote. Vitu kama skauti, jeshi la kujenga taifa pia vina nafasi yake katika hili.


Yas, mifumo iwekwe sawa kukabiliana na chochote wakati wowote. Tujiulize na tuiulize serikali: au hili la watu kutojiandaa vema ni 'dili' ili kupata nafasi ya kuchota pointi muhimu kwa kuonesha matendo ya huruma kwa wahanga?
Hilo la mwisho linafikirisha sana ase!!
 
Back
Top Bottom