Atheists wana mtindio wa ubongo

Siyo kwa makusudi kivipi ? Taka hao viumbe wanao otesha si kwa makusudi na ututhibitishie Hilo.

Kingine unaposema uuthibitisho upo na huuweki hayo ni matumizi mabaua ya akili.

Kitu gani naamini hakina Proof hata moja. Kila siku nawakanya, acheni kuongelea mambo ambayo hamna Elimu nayo, matokeo yake ni haya kuandika andika hovyo na kuzua uongo.

Kuna uongo kule nyuma kuhusu Mtume alishika mwezi kaufute.
 
Kijana nilikuuliza kuhusu maana ya Roho hukutoa maana, unajua maana ya maana ? Au unaleta utoto ? Hujajibu swali langu, uliandika tu Imani mara myth yaani unaruka ruka, ajabu unadai hakuna Roho na kuielezea roho hujui huu ni upunguani yaani akili zenu zina matatizo.
Jibu swali nililo kuuliza.

Sababu kadhia ya Cloning naijua, hiyo mifano yako unayo dai Iko mingi haithibitishiki, ndiyo maana nimekuomba mmoja tu Kisha nikuulize maswali.
 
Hata hujui ulichojibu
Uhalisia ndio huu sisi tunaojaribu kukuonyesha.

Ili tukutoe tongotongo kwenye macho yako na uijue kweli.
Uhalisia gani ambao umenionyesha kijana ? Itakuwa hujui maana ya Uhalisia.

Hakuna uhalisia ambao unaweza kunionyesha japo upo ni kukuchukua tu. Mnaacha uhalisia mnamfata fikra zenu.

Jibu maswali ninayo kuuliza, utajua maana ya Uhalisia, Roho ni nini ? Unaposema kitu Fulani hakipo, maana yake una ujuzi juu ya kitu hicho, Sasa hata Roho huijui lakini unadai haipo. Halafu unajinadi unaonyesha Uhalisia ? Roho yenyewe ni uhalisia.
 
Kijana kama hujibu maswali ninayo kuuliza. Haina maana ya mjadala. Nimekuomba uthibitisho wa hao Wajapani unaleta stori.

Kuhusu Mimi kuona vitu vya Past kwa mtindo gani ? Au kwa msaada wa nini ?
Nimeonesha mbinu wanazotumia kupredict earthquakes...

Ukiangalia nyota usiku, baadhi yake ziko mamilioni ya light years away. '1 million light years away' inamaana kufika huko kwa speed ya mwanga, utatumia miaka 1mil. Na ili uone kitu inamaana mwanga unasafiri kutoka ktk object mpaka machon kwako. Ivo kuona kitu kilichopo 1mil light years away, inamaana unakiona kilivokua miaka hio iliopita. Kwahio jua nalo unapoliangalia unaliona dakika 8 zilizopita...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna uthibitisho wa watu kutengeneza rain cycle yao? Saudis are doing just that! Afu unasema et hio sio 'mvua'. Wakat formation yake na kila kitu ni mvua kabisa.. mbona na hilo unalipinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeshaelezea nini maana ya roho.
Kama Ina walakini leta ya kwako utakayo hisi imekamilika.

Unaponiita kijana? Je wafahamu lika langu?

Usitumie kiswahili kingi kama janja ya Nyani unachokisoa ni nini Sasa?

Je, Human Cloning haiwezekani au haijafanyika?

Je, Wanyama wengine hawafanyiwi?

Leta maswali yako, nami nitayajibu
Karibu
 
Wewe usipofata fikra zako, unafuata fikra za nani?

Uhalisia ndio huu yaani hakuna roho.

Roho ni myth iliyoanza kutumika kipindi Cha maendeleo duni ya kisayansi kwenye jamii.

Kama unabisha roho ni nini?
Taja sifa za roho?
Nini tofauti ya pumzi na roho.
View attachment 2530461
 
Tetemeko ni janga la asili (nature), na haliathiriwi na uovu au dhambi. Dhambi au uovu havitengenzi tetemeko hata kidogo. Tetemeko linaathiri maovu yaliyotendeka na binadamu. Hapo sina shaka umeelewa.

Uovu/dhambi ni kujenga nyumba chini ya viwango sahihi. Tetemeko lisingeathiri kitu kama nyumba zingejengwa kwa viwango sahihi. Nyumba zilizojengwa kwa viwango sahihi hazikupata madhara.

Mungu yuko perfect, hana dosari na ana upendo. Aliumba dunia kwa jinsi ilivyo likiwemo na tetemeko. Mungu alitupa akili za kukabiliana na majanga mbalimbali likiwemo la tetemeko. Hayo yote yalifanyika kwa upendo ili tuweze kuishi kwa furaha katika dunia hii. Kama binadamu tutatumia akili zetu kwa usahihi, majanga kama hayo hayatatuhusu.

Ni kweli kabisa Mungu anayachukia mabaya kwa kuwa yeye hafanyi mabaya. Yanafanywa na binadamu.
Ili tuepukana na mabaya ya dunia, ni lazima matumizi yetu ya akili yawe sahihi. Nguvu ya ushindi ameiweka kwenye akili yako. Ukishindwa utakuwa umeamua mwenyewe.
 
Tetemeko ni janga la asili (nature), na haliathiriwi na uovu au dhambi. Dhambi au uovu havitengenzi tetemeko hata kidogo. Tetemeko linaathiri maovu yaliyotendeka na binadamu. Hapo sina shaka umeelewa.
Unaposema tetemeko lina athiri uovu au dhambi unakusudia nini?

Kwasababu tunawaona watu wakifa kuliko huo uovu unaousema wewe

Husuani pale tunapoona vifo hadi vya watoto wadogo wasio na hatia

Au ule uharibifu wa majengo ndio uovu wenyewe?
 
Uovu/dhambi ni kujenga nyumba chini ya viwango sahihi. Tetemeko lisingeathiri kitu kama nyumba zingejengwa kwa viwango sahihi. Nyumba zilizojengwa kwa viwango sahihi hazikupata madhara.
We jamaa ni comedian sana

Kwa hiyo Mungu hakuridhishwa na kazi za uinjinia na kwamba kitendo hicho kwake kilikuwa kama ni dhambi kubwa sana ambayo adhabu yake ni kuangamiza waelfu ya watu (ambao sio wajenzi wa hizo nyumba) ikiwemo na watoto wadogo?

Is this how you choose to defend your God?
 
No. Logic inakataa kuwa na Mungu mwenye upendo wote anayeua maelfu ya watu iliwemo watoto, kwasababu ya kipumbavu "kutoridhishwa na miundombinu iliyojengwa chini ya kiwango"

Huyo ni Mungu wa kufikirika tu
 
Anayachukia mabaya, ila hana uwezo wa kuyadhibiti yasiwepo?

Kama jibu hapo litasema ana uwezo

Then how come mabaya yapo?

Basi sio kweli kuwa hapendi mabaya yawepo unless tukubaliane kuwa hana uwezo wakufanya yasiwepo

Au ana uwezo na aliweza kuyadhibiti ila hakutaka

Then hawezi kuwa Mungu mwema mwenye upendo wote kwa viumbe wake
 
nikuulize atheits umekutana nao wapi?
 
No. Logic inakataa kuwa na Mungu mwenye upendo wote anayeua maelfu ya watu iliwemo watoto, kwasababu ya kipumbavu "kutoridhishwa na miundombinu iliyojengwa chini ya kiwango"

Huyo ni Mungu wa kufikirika tu
Mwalimu safi huwa anaiga tabia za Mungu. Anafundisha kwa usahihi ili kutoa majibu sahihi wakati wa mthani. Sio kazi ya mwalimu kukupa majibu sahihi wakati wa mtihani. Kama hukuzingatia utakumbwa na tetemeko la kufeli.

Hata Mungu pia ametupa akili sahihi za kufanya mambo kwa usahihi. Tusipozingatia, tunapata matatizo. Sio jukumu la Mungu kutupa majibu ya viwango sahihi vya ujenzi wa nyumba sahihi dhidi ya tetemeko. Ujenzi wetu ni majanga, na mchuma janga hula na wa kwao. Watoto wamekufa kwa sababu sisi tumechuma janga. Inasikitisha sana.

Mungu yupo si wa kufikirika.
 
Swala la kupata matatizo kwasababu hujazingatia ni jambo la mbeleni

Hoja yangu imejikita kuhoji mwanzo kabisa wakati Mungu anaumba ulimwengu

Aliumba bila kujua kuwa ulimwengu huu una imperfections za kuweza kuruhusu mabaya?

Kama jibu ni hapana, basi ubaya unaofanyika saizi ni Mungu alitaka uwepo kwasababu aliuona mwanzo kuwa utaweza kufanyika lakini akauacha (kwasababu alikuwa na uwezo wa kuzuia)

Kwa hiyo kila kitu ambacho kinafanyika hapa kimepewa kibali na Mungu na Binadamu hawezi kupewa lawama, kwasababu Mungu ndio ametaka iwe hivyo.

Na kwasababu ametaka iwe hivyo, ikiwemo kuruhusu mabaya basi hawezi kuwa Mungu mwema au mwenye upendo wote kwa viumbe wake
 
Unaposema tetemeko lina athiri uovu au dhambi unakusudia nini?

Kwasababu tunawaona watu wakifa kuliko huo uovu unaousema wewe

Husuani pale tunapoona vifo hadi vya watoto wadogo wasio na hatia

Au ule uharibifu wa majengo ndio uovu wenyewe?
Nina maana kuwa tetemeko limeathiri kazi dhaifu ya mikono ya binadamu. Kazi dhaifu ndiyo uovu na dhambi yenyewe. Kazi dhaifu imeathiri maisha ya watu.

Mungu hahusiki na ubovu wa nyumba zilizoathirika. Mungu alitupa uwezo wa akili za kujenga nyumba imara, lakini hatukufanya hivyo.

Kule kujenga nyumba chini ya kiwango ndiyo dhambi yenewe. Tetemeko limeathiri dhambi ya ujenzi dhaifu na ujenzi dhaifu umearhiri maisha binadamu.
 
Watoto wadogo waliokufa nao ni sehemu ya kazi dhaifu za mikono ya binadamu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…